Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Sunday, 13 July 2014

BENKI YA CRDB YAWASHAURI WAZAZI KUWAFUNGULIA WATOTO AKAUNTI YA JUNIOR JUMBO

Benki ya CRDB imewataka wazazi kuwafungulia watoto akaunti ya Junior Jumbo kwa ajili ya akiba yao ya baadae.

Akizungumza katika maonyesho ya 38 ya Biashara ya Taifa Jijini Dar es Salaam, Afisa Masoko wa CRDB Bank, Nazareth Kipingo, alisema akaunti hiyo ni kwa ajili ya watoto ambapo mzazi huhifadhi fedha kwa ajili ya ada au akiba ya mtoto katika maisha yake ya baadae.

Alisema akaunti hiyo itamsaidia mzazi kuweka fedha kimkakati ambapo atatakiwa kutoa mara nne kwa mwakakatika msimu wa ada ya shule na kuongeza kuwa CRDB inaweza kumlipia mtoto ada kwa utaratibu maalum.

Kipingo alisema Junior Jumbo ni akaunti inayomhakikishia mtoto elimu ya uhakika na kupunguza kero za kulipa ada kwa mkupuo kutoka mfukoni mwa mzazi.

Alisema kuwa katika maonyesho hayo, wanaendesha huduma za kibenki katika viwanja hivyo ili kumpunguzia mteja adha ya kutembea na pesa.

Mteja mtarajiwa wa Benki ya CRDB akijaza fomu kwa ajili ya kufungua akaunti.

Watu mbalimbali walifurika katika banda la Benki ya CRDB kwa ajili ya kufungua akaunti mpya pamoja na kupata huduma mbalimbali za kibenki zinazotolewa na Benki ya CRDB. 

Wateja wa Benki ya CRDB wakipata huduma za kibenki kutoka katika tawi linalotembea (Mobile Branch), wakati wa maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yaliyofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere, Jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment