Blog Rebranding Teaser_030826

Blog Rebranding Teaser_030826

Stanbic Bank Banner_070826

Stanbic Bank Banner_070826

Absa Loan Campaign_160426

Absa Loan Campaign_160426

Monday, 5 May 2025

BENKI YA NMB YAPANIA KUIINUA TEHAMA UDOM


Benki ya NMB na Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) wametiliana saini Mkataba wa makubaliano (MoU) juu ya ushirikiano katika kukuza uwezo wa kiteknolojia na Tehama kwa lengo la kushirikiana katika kukuza bunifu.


Mkataba huo unalenga kukuza uwezo wa Watanzania katika masuala ya kitehama lakini pia kuendelea kuchochea mabadiliko makubwa ya kidigitali yanayohusiana na sekta ya fedha.


Afisa Mkuu Rasilimali watu wa Benki ya NMB, Emmanuel Akonaay ameongoza timu ya wataalamu wa Benki hiyo katika kutiliana saini huku Chuo kikuu cha Dodoma kikiongozwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu hicho, Profesa Lughano Kusiluka.


Akizungumza kuhusu mpango huo, Akonaay amesema katika makubaliano hayo wanalenga kuibua na kuendeleza vipaji mbalimbali ili kubaini wanafunzi wanaofanya vyema zaidi katika fani ya Tehama (ICT).


Amesema NMB itawapatia ushauri na kuwakuza kiuwezo, kuwapatia nafasi ya mafunzo kwa vitendo na kuwapa fursa ya kutekeleza mawazo walionayo, lakini kutoa mafunzo kwa kampuni changa kupitia programu za kuongeza ujuzi yaani (accelerator program).


Akonaay amesema kupitia mpango huo, wanafunzi wa UDOM watapata jukwaa maalum la kufanya majaribio ya bunifu za kiteknolojia zitakazokuwa na mrengo wa masuala ya kifedha na kuwapa fursa za kuendelea kubuni teknolojia katika sekta ya fedha (kwa mfumo wa NMB Sandbox).


Amesema hadi sasa kuna wabunifu zaidi ya 300 ambao wamejisajili katika mfumo wa sandbox wanaofanya tafiti za bunifu zao ikiwemo wanafunzi na kampuni changa za tehama yaani startups ambazo wanategemea kuziunga kwenye mfumo wa kibenki.


Kwa kufanya hivi, Benki ya NMB inalenga kuhimiza na kukuza tamaduni ya kuja na teknolojia zinazohamasisha ujasiriamali lakini pia utatuzi wa changamoto mbalimbali katika sekta hii ya fedha,” amesema.


Kwa mujibu wa kiongozi huyo, Benki ya NMB inaamini katika mabadiliko ya kidigitali ndiyo maana wamewekeza huko hivyo matamanio yao ni kuona wanafunzi kutoka UDOM wakiwa mstari wa mbele katika safari ya mabadiliko ya kidigitali.


Kwa upande wa elimu ya Fedha amesema NMB inatambua umuhimu wake elimu ya fedha kwa vijana wetu, tutaendelea kutoa elimu ya fedha ili kuweza kuwafanya wanafunzi, walezi na wazazi kuwa na uelewa kuhusu masuala ya kifedha na kuweza kufanya maamuzi sahihi ya fedha kila wakati na hii itasaidia katika nyanja mbalimbali za kimaisha kwani ni muhimu kufahamu vitu kama Bajeti na uwekezaji ulio bora wa fedha zako.

NMB BANK & UNIVERSITY OF DODOMA PARTNER TO PROPEL TECHNOLOGICAL INNOVATION



NMB Bank and the University of Dodoma (UDOM) have signed a Memorandum of Understanding (MoU) to collaborate in enhancing technological and ICT capabilities, with a mutual aim of fostering innovation.


This agreement seeks to bolster the technological expertise of Tanzanians while also driving significant digital transformations in the financial sector. The signing ceremony was led by NMB Bank’s Chief Human Resources Officer, Emmanuel Akonaay, and the Vice Chancellor of UDOM, Professor Lughano Kusiluka.


Discussing the plan, Akonaay stated that the agreement aims to cultivate and develop various talents, especially identifying students excelling in the field of ICT. NMB Bank plans to provide expert advice, capacity-building opportunities, hands-on training, and platforms to implement their ideas. They will also offer training through accelerator programs to support startups.


Through this initiative, UDOM students will gain access to a specialized platform to test technological innovations with a financial focus, offering them the chance to continue developing innovations in the financial sector via the NMB Sandbox framework.


Currently, over 300 innovators, including students and tech startups, are registered in the sandbox program, conducting research and development on their innovations with the expectation of integrating them into the banking system.


By doing this, NMB Bank aims to encourage a culture of entrepreneurial technology development while also addressing various challenges within the financial sector,” Akonaay remarked.


According to the bank executive, NMB Bank believes in digital transformation, which is why they have invested significantly towards this. Their ambition is to see UDOM students leading the digital change journey.


On financial education, NMB underscores its importance for youth and commits to continue providing financial literacy programs to help students, guardians, and parents make informed financial decisions consistently, aiding in various life aspects, including budgeting and optimal investment of finances.


Professor Lughano Kusiluka of UDOM commented that the agreement awaits enthusiastic participation from students, university leadership, and NMB Bank, which could boost technological growth in the country and across Africa.

KONGAMANO LA KIMATAIFA LA UWEKEZAJI KUFANYIKA ZANZIBAR JUNI 13-15, 2025

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA), Saleh Saad Mohamed, akizungumza juu ya kusogezwa mbele kwa Kongamano la Kimataifa la Uwekezaji Zanzibar ambalo sasa litafanyika Juni 13 mpaka 15 mwaka huu.

Mkutano mkubwa wa uwekezaji utakaowakutanisha wawekezaji na wafanyabiashara mbalimbali kutoka nchi mbalimbali Afrika utafnyika, Pemba, Zanzibar kuanzia Juni 13 mpaka Juni 15 katika viwanja vya uwekezaji, Micheweni, Pemba mwaka huu.

Awali mkutano huo ulipangwa kufanyika Mei 7 mwaka huu lakini waandaaji, Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) imetangaza kuusogeza mbele mkutano huo kwa mwezi mmoja kutokana na maombi ya wafanyabiashara wengi.

Akizungumza kutoka Zanzibar, Mkurugenzi Mtendaji wa ZIPA, Saleh Saad Mohamed, alisema pamoja na watu wengi kujiandikisha kushiriki Mkutano huo, bado yapo mapombi mengi ya wafanyabisahara wengine wa ndani na nje ya nchi waliomba kusogeza mbele ili kuwapa nafasi ya kujiandikisha na kuiandaa kushiriki.

"Nichukue fursa hii kuwaomba wafanyabisahara na wananchi kutumia kipindi hiki kujiandikisha kushiriki katika kongamano hili, kwa pamoja tunawaomba mjitokeze kwa wingi kuangalia fursa za uwekezaji Pemba," alisema

Aidha, alisema ratiba nyingine ya mkutano huo ipo kama ilivyopangwa ambapo Rais wa Zanzibar, Hussein Mwinyi, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kufungua mkutano huo mkubwa wa masuala ya uwekezaji na biashara.

PROHIBITION OF FOREIGN CURRENCY USE FOR LOCAL TRANSACTIONS IN TANZANIA

EXIM BANK STARTS 2025 STRONG WITH BOLD GROWTH PLANS AHEAD


Dar es Salaam, 
May 2, 2025: Exim Bank Tanzania has reported a strong start with its first quarter of 2025, underlining its continued growth momentum, operational efficiency, and impactful initiatives that align with its long-term strategy for innovation and inclusion. For the period ended 31st March 2025, the bank posted strong financial metrics across the board, reinforcing its role as one of Tanzania’s leading private sector financial institutions.

The bank’s total assets rose to TZS 3.4 trillion, marking an 18.2% increase compared to the same period last year. Net Loans and advances also surged to TZS 1.9 trillion, representing a 20% year-on-year growth. The strong lending performance reflects the bank’s commitment to supporting both individuals and enterprises across key economic sectors.

Moreover, profit before tax for the first quarter of 2025 reached TZS 26.5 billion, marking a strong performance that underscores the bank’s disciplined execution of its strategic priorities. This growth reflects the success of its customer-first approach, prudent risk management, and continued investment in innovative financial solutions that respond to the evolving needs of individuals and businesses across Tanzania.

Total customer deposits reached TZS 2.7 trillion, a 20% increase from the previous year, demonstrating growing trust in the bank’s ability to deliver value-driven and customer-focused banking solutions. Net interest income for the quarter stood at TZS 43.7 billion, a 7% increase year-on-year, underpinned by improved asset quality and a resilient lending strategy.

Commenting on the performance, Exim Bank’s Chief Financial Officer, Shani Kinswaga said, “We are pleased with our Q1 2025 performance, which not only shows solid financial growth but also the tangible impact of our commitment to inclusion and innovation. Our focus remains on delivering accessible, digital-first, and customer-friendly banking experiences that support Tanzania’s economic transformation.”

Friday, 2 May 2025

AFISA MTENDAJI MKUU, DSE AFANYA MAZUNGUMZO NA WAZIRI MKUU KUHUSU UWEZESHAJI WA MIRADI



Dodoma, Mlimwa, 27.04.2025: Afisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa Dar es Salaam, Bw. Peter Nalitolela atembelea Ofisi ya Waziri Mkuu na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim M. Majaliwa (Mb.) ambapo waligusia juu ya Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE) kuwezesha serikali, mashirika, halmashauri na manispaa za miji kupata fedha zaidi za kukamilisha miradi, lakini pia alisisitiza utolewaji wa elimu kwa Umma juu ya fursa zilizopo DSE ili kuweza kufanikisha lengo la serikali katika sera ya uchumi jumuishi.

#DSE
#WaziriMkuuBingwa
#MiradiYaMendeleoe
#UstawiWaJamii
#TanzaniaImara
#DSEHisaKiganjani

BENKI YA CRDB YASHIRIKI MAADHIMISHO YA MEI MOSI, SINGIDA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Naibu Waziri Mkuu, Dkt. Dotto Biteko na Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), Tumaini Nyamhokya kwa pamoja wakiwa wameshikana mikono wakati wakiimba wimbo wa mshikamano kwenye maadhimisho ya Sherehe za Wafanyakazi (Mei Mosi) yaliyofanyika kitaifa, katika viwanja vya Bombadia mkoani Singida.

Kwenye maadhimisho hayo, Benki ya CRDB ambayo ni Mwajiri Bora zaidi nchini, iliungana na Watanzania pamoja na dunia nzima kusherehekea mchango wa wafanyakazi katika kukuza uchumi.

Benki hiyo iliwakilishwa na viongozi kutoka Makao Makuu pamoja na wafanyakazi kutoka makao makuu, kanda ya kati na matawi ya Singida wakiongozwa na Afisa Mkuu wa Fedha, Fredrick Nshekanabo aliyesindikizwa na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu, Godfrey Rutasingwa.


Afisa Mkuu wa Fedha, Fredrick Nshekanabo (watano kushoto) akiwa na wageni wengine kwa pamoja wakiwa wameshikana mikono wakati wakiimba wimbo wa mshikamano kwenye maadhimisho ya Sherehe za Wafanyakazi (Mei Mosi) yaliyofanyika kitaifa, katika viwanja vya Bombadia mkoani Singida.

Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakipita mbele ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzinia, Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa maadhimisho ya Mei Mosi yaliyofanyika kitaifa katika viwanja vya Bombadia Mkoani Singida.

Magari ya Benki ya CRDB yakiwemo Matawi yanayo tembea yakishiriki katika maadamano ya Mei Mosi yaliyofanyika katika viwanja vya Bombadia Mkoani Singida.






Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akiwapungia wafanyakazi waliokuwa wakipita kwa maandamano mbele yake wakati wa maadhimisho ya Sherehe za Wafanyakazi (Mei Mosi) yaliyofanyika kitaifa, katika viwanja vya Bombadia mkoani Singida.




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akihutubia wakati wa maadhimisho ya Sherehe za Wafanyakazi (Mei Mosi) yaliyofanyika kitaifa, katika viwanja vya Bombadia mkoani Singida.


Afisa Mkuu wa Fedha, Fredrick Nshekanabo (katikati) akiwa na wageni wengine kwenye maadhimisho ya Sherehe za Wafanyakazi (Mei Mosi) yaliyofanyika kitaifa, katika viwanja vya Bombadia mkoani Singida.

BENKI YA NBC YASHIRIKI MAADHIMISHO MEI MOSI SINGIDA



Singida; Mei 2, 2025: Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeungana na mamilioni ya wafanyakazi kote nchini na duniani kwa ujumla kusherekea Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, Mei Mosi ambayo kitaifa yamefanyika kwenye Viwanja vya Bombadia Mkoani Singida, yakiongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.


Maadhimisho hayo yaliyohusisha wafanyakazi na viongozi wengine waandamizi akiwemo Dkt. Philip Isdor Mpango, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Ridhiwani Kikwete yaliratibiwa na Shirikisho la Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali vikiwemo vyama tofauti vya wafanyakazi. Benki ya NBC ilikuwa kuwa moja ya wadhamini muhimu wa maadhimisho hayo.


Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Mahusiano ya Umma wa Benki ya NBC Bw Godwin Semunyu aliwaongoza wafanyakazi wengine wa benki hiyo kusherehekea siku hiyo muhimu akiwa sambamba na Mkuu wa Kanda ya Kati wa benki ya NBC, Bw Miraji Msuya na Meneja wa NBC tawi la Singida Bw David Mushi.


Bw Semunyu alisema ushiriki wa benki hiyo kwenye maadhimisho hayo unatokana na kutambua umuhimu wa siku hiyo kwa wafanyakazi ambao ni nguzo muhimu katika ustawi na ukuaji wa uchumi wa nchini huku benki hiyo ikichangia ukuaji huo kupitia huduma mbalimbali za kibenki inazozitoa kwa wafanyakazi hao na serikali kwa ujumla.


Katika maadhimisho haya NBC tunaungana na mamilioni ya wafanyakazi wenzetu kote nchini kusheherekea siku hii muhimu sana kwetu sote, kwanza tukiwa kama wafanyakazi, pili tukiwa wadhamini muhimu katika kufanikisha uratibu wa maadhimisho haya na tatu tukiwa kama watoa huduma za kifedha kwa wafanyakazi kupitia matawi yetu yaliyopo kote nchini ikiwemo hapa Singida pamoja na kupitia kwa maelfu ya mawakala wetu kote nchini,’’ alisema.


Kwa mujibu wa Bw Semunyu, ushirikiano wa benki hiyo na wafanyakazi unaimarishwa zaidi kupitia huduma za benki hiyo zinazotolewa kwa kundi hilo kwa kuzingatia mahitaji yao mahususi ikiwemo kuwatunzia amana zao kupitia akaunti mbalimbali kulingana na machaguo yao pamoja na kuwarahishia miamala.

Thursday, 1 May 2025

NMB YADHAMINI NA KUSHIRIKI MAADHIMISHO YA MEI MOSI KITAIFA – SINGIDA



Benki ya NMB imedhihirisha tena nafasi yake kama Mwajiri Kinara nchini kwa kudhamini na kushiriki kikamilifu katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi), yaliyofanyika kitaifa mkoani Singida.


Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na maelfu ya wafanyakazi kutoka sekta mbalimbali nchini, yakiwemo mashirika ya umma na binafsi, taasisi na vyama vya wafanyakazi, yakilenga kuenzi mchango wa wafanyakazi katika maendeleo ya taifa.


Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, akiambatana na viongozi waandamizi wa Serikali na wageni mbalimbali waalikwa.


Ujumbe wa NMB katika maadhimisho hayo umeongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo, Bi. Ruth Zaipuna, akiwa na baadhi ya viongozi wakuu na wafanyakazi wa benki hiyo walioungana na wenzao kuadhimisha siku hiyo muhimu.


Kupitia ushiriki wake, NMB imesisitiza dhamira yake ya kuendelea kuwekeza katika ustawi wa rasilimali watu, kuboresha mazingira ya kazi na kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuboresha sekta ya ajira nchini.


Benki hiyo pia imewatakia wafanyakazi wote nchini maadhimisho mema ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, ikiwa ni sehemu ya kutambua na kuthamini mchango wao mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa taifa.