Blog Rebranding Teaser_030826

Blog Rebranding Teaser_030826

Stanbic Bank Banner_070826

Stanbic Bank Banner_070826

Absa Loan Campaign_160426

Absa Loan Campaign_160426

Friday, 20 September 2024

BENKI YA NMB WAPIGA TAFU MASHINDANO YA KIMATAIFA YA DIPLOMATIC GOLF


Arusha: Benki ya NMB imefanikiwa kukabidhi udhamini wa vifaa vya michezo kwa ajili ya wachezaji 150 wanaotarajia kushiriki mashindano ya kimataifa ya Diplomatic Golf 2024.


Michuano hiyo inayotarajia kuanza kutimua vumbi kwa siku mbili kuanzia Septemba 21-22, 2024 katika viwanja vya Kili Golf vilivyoko Mkoani Arusha yana lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia watoto wanaotoka katika mazingira magumu.


Mashindano hayo yaliyoandaliwa na Taasisi ya Songea Mississippi (SOMI) na klabu mwenyeji ya Kili Golf, jumla ya mashimo 36 yataamua mshindi kutoka kwa washiriki wote 150 kutoka nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na wachezaji kutoka Dubai na Marekani.


Mratibu wa mashindano hayo, Reinfrida Rwezaura, amesema kuwa maandalizi yote kuelekea mashindano hayo ya msimu wa sita mwaka huu yamekamilika.


Amesema lengo kuu la mashindano hayo ni kukusanya fedha kwa ajili ya kusaidia vituo vya kulelea watoto yatima na kuwasaidia wale wenye uhitaji, ikiwa ni pamoja na kusaidia wasichana wajawazito kurudi shule.


Pia mashindano haya yanatoa jukwaa la wachezaji kuonyeshana makali yao katika mchezo wa Gofu kutoka mikoa na nchi mbalimbali, pia yanatoa fursa kuonyesha ujuzi wao na nidhamu ya michezo lakini pia ya yanachangia jitihada za nchi za kukuza utalii kupitia michezo.

NMB YAJITOSA KUIDHAMINI YANGA DHIDI YA CBE CAF CL 2024/25


Kuelekea pambano la marudiano raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF CL 2024/25), dhidi ya CBE ya Ethiopia, mabingwa wa Tanzania, Yanga wameitambulisha Benki ya NMB kuwa ni mmoja wa wadhamini wa mechi hiyo, ushirikiano uliopewa jina la ‘Timu Bora, Benki Bora’.


Yanga wanashuka dimbani Jumamosi ya Juni 21 kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar, kuumana na Wahabeshi hao, wakiwa na uongozi wa bao 1-0 waliopata katika mechi ya kwanza jijini Addis Ababa, Ethiopia na mshindi wa jumla atafuzu hatua ya makundi ya michuano hiyo.


Akizungumza wakati wa hafla ya utambulisho wa wadhamini wa mechi hiyo, Meneja Biashara wa NMB Zanzibar, Bi. Naima Said Shaame, alisema siri ya uamuzi wao wa kujitosa kuidhamini Yanga ni mvuto ilionao klabu hiyo, unaoakisi mafanikio makubwa katika soka kitaifa na kimataifa.


“Tumevutiwa na mafanikio ya klabu hii, tukaona ipo haja ya Timu Bora kupewa nguvu na Benki Bora. Wametoka kutwaa Ngao ya Jamii katika ufunguzi wa msimu huu, lakini katika Ligi ya Mabingwa Afrika, wamefuzu raundi hii kwa kishindo baada ya kuwachapa Vital’O ya Burundi kwa jumla ya mabao 10-0.

“Kwa kutambua ukubwa wa Yanga, tukalinganisha na ukubwa wa NMB, tukaona ipo haja ya kuwasapoti katika mechi dhidi ya CBE itakayopigwa hapa wikiendi hii na leo tuko hapa kutambulishwa rasmi washirika wa Yanga kuelekea mechi ya CBE,” alisema Bi. Naima.

NMB BANK REITERATES COMMITMENT TO SUPPORT LOCAL MSMEs


NMB Bank has reiterated support for Micro, Small, and Medium Enterprises (MSMEs) across the country as part of its commitment to drive increased growth and development.


Speaking during an event to the launch of the Kariakoo Festival held in Dar es Salaam that brought together 100 exhibitors from both public and private sector, the NMB Bank’s Head of Business Banking, Alex Mgeni said his bank will continue to play a leading role in the economic transformation and growth of MSMEs.


Mgeni said the Kariakoo business hub remains a pivotal and strategic business hotspot for the bank adding that the festival provides a platform for the bank to engage directly with its clients and aligns with the bank’s quest to businesses to the next level.


“We did not have second thoughts when contacted to be sponsors for the Kariakoo Festival. At NMB Bank, we believe MSMEs are the primary drivers of economic development. We have implemented a comprehensive suite of initiatives including seamless digital payment propositions such as NMB Mkononi tailored to meet the varied needs of entrepreneurs,” he stressed.


Mgeni said apart from providing funding for MSMEs, the bank also enhanced their capacities by providing financial literacy and creating networking opportunities for them.


“We are confident that our continued support for MSMEs will lead to an improvement in their performance and contribution to the economy as a whole,” he noted.


The Dar es Salaam Regional Administrative Secretary (RAS) Dr. Toba Nguvila commended the bank for sponsoring the event adding that the idea for the event was masterminded by the Kariakoo business community which is committed to see businesses thrive.


“Kariakoo market is arguably East and Central Africa's most vibrant commercial hub. This is an international market and in a bid to move in line with this status, it has begun providing services 24hrs now. We are proud of the Kariakoo Festival and we believe it will showcase various goods available to the world,” He added.


Tuesday, 17 September 2024

NMB DONATES MEDICAL SUPPLIES TO SUPPORT HEALTH SECTOR IN MAKETE DISTRICT


As part of its efforts to boost healthcare service delivery, NMB Bank donated medical equipment including beds and bed sheets to the Ivilikinge Village Dispensary in Makete District, Njombe Region worth 9m/-.


Speaking during the handover ceremony held over the weekend, NMB Bank Acting Manager for the Southern Highlands Zone, Willy Mponzi, reiterated the bank's commitment to supporting development of the health sector adding that the bank through its Corporate Social Investment (CSI) strategy allocates one percent of its Profit After Tax each year to support various development initiatives in its key priority areas.


"This donation in Makate today aligns with our CSI strategy. As a bank, we are committed to supporting development of the health sector as we believe a healthy mind lives in a healthy body. We believe these medical supplies will go a long way in enhancing service delivery here,” he stressed.

He added that the bank had initially contributed roofing materials worth 8m/- during the construction phase of the dispensary.

He noted that the bank has for several years been actively involved in in supporting the education sector as well by providing desks and roofing materials as part of its commitment to support the sector’s development.

STANBIC YATOA SH. MIL. 70 KWENYE ZIARA YA BAISKELI YA VODACOM TWENDE BUTIAMA 2024

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Stanbic Tanzania, Manzi Rwegasira, akizungumza wakati wa uzinduzi wa ziara ya waendesha baiskeli kuelekea Butiama 2024, ambayo inadhaminiwa na Vodacom Foundation kwa kushirikiana na Benki ya Stanbic. Uzinduzi huu ulifanyika kama maendesho ya baiskeli ya kijamii "Pedal for Purpose," ambayo ni mwanzo wa ziara hii kuelekea Butiama. Benki ya Stanbic imechangia kiasi cha shilingi milioni 70, ambazo zitatumika kuboresha sekta ya elimu kwa kutoa madawati 1,500; sekta ya afya kwa kuanzisha kliniki zinazozunguka kuhudumia mikoa mbalimbali, na utunzaji wa mazingira kwa kupanda miti 50,000. Kiujumla ziara hii inategemea kuboresha maisha ya watanzania 100,000. Kilele cha ziara hiyo kitafanyika Butiama, Mkoani Mara, tarehe 14 Oktoba.
Mchezaji wa zamani kutoka Nigeria - Nwankwo Kanu (kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania - Philip Besiimire (katikati) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Stanbic Tanzania - Manzi Rwegasira wakifuatilia jambo wakati wa uzinduzi Vodacom Twende Butiama 2024 uliofanyika jijini Dar es salaam.





Mchezaji wa zamani kutoka Nigeria - Nwankwo Kanu (katikati), Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania - Philip Besiimire (kushoto) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Stanbic Tanzania - Manzi Rwegasira (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja.

MASHINDANO YA TANZANIA LADIES OPEN GOLF TOURNAMENT 2024 YAHITIMISHWA ARUSHA

Wadau mbalimbali wa mchezo wa gofu wakiwemo washindi wa mashindano ya gofu ya Tanzania Ladies Open Golf Tournament wakijipongeza na zawadi zao wakati wa hafla fupi ya kuhitimishwa kwa mashindano hayo ya siku tatu yaliyohitimiswa mwishoni mwa wiki jijini Arusha. Benki ya NBC ilikuwa mdhamini Mkuu wa mashindano hayo yaliyofanyika kwenye viwanja vya klabu ya gofu ya Gymkhana jijini Arusha.
Meneja Mahusiano wa Benki ya NBC, Bw. Gerald Tarimo (katikati) pamoja na Rais wa Chama cha Gofu cha Wanawake Tanzania (TLGU), Bi. Queen Seraki (wa pili kushoto) wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya washiriki na washindi wa mashindano ya gofu ya Tanzania Ladies Open Golf Tournament akiwemo mshindi wa jumla, Mercy Nyanchama kutoka nchini Kenya (wa tatu kushoto) wakati wa hafla fupi ya kuhitimishwa kwa mashindano hayo ya siku tatu yaliyohitimiswa mwa wiki jijini Arusha. Benki ya NBC ilikuwa mdhamini Mkuu wa mashindano hayo yaliyofanyika kwenye viwanja vya klabu ya gofu ya Gymkhana jijini Arusha.
Meneja Mahusiano wa Benki ya NBC, Bw. Gerald Tarimo (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya washiriki na washindi wa mashindano ya gofu ya Tanzania Ladies Open Golf Tournament wakati wa hafla fupi ya kuhitimishwa kwa mashindano hayo ya siku tatu yaliyohitimiswa mwa wiki jijini Arusha.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Rais wa Chama cha Gofu cha Wanawake Tanzania (TLGU), Bi. Queen Seraki (pichani) pamoja na kuwapongeza washiriki na washindi mbalimbali wa mashindano hayo wakiwemo wale waliotoka nje ya nchi, pia aliwashukuru wadau mbalimbali waliofanikisha mashindano akiwemo mdhamini mkuu wa mashindano hayo Benki ya NBC.
Akizungumza kwenye hafla fupi ya kukabidhi zawadi kwa washindi mbalimbali wa mashindano hayo, Meneja Mahusiano wa Benki ya NBC, Bw. Gerald Tarimo pamoja na kuwapongeza washiriki pamoja na washindi mbalimbali wa mashindano hayo alisema benki hiyo itaendelea kuyaunga mkono ikiwemo kuyaboresha zaidi ikiwa ni sehemu ya jitihada zake katika kuchochea ushiriki wa wanawake katika michezo.


Arusha; Septemba 17, 2024 - Mashindano ya siku tatu ya Gofu ya Tanzania Ladies Open Golf Tournament yamehitimswa mwishoni mwa wiki jijini Arusha huku wadhamini wakuu wa mashindano hayo, Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) wakiahidi kuendelea kuyaboresha zaidi mashindano hayo ili kuyoangozea ubora na ushindani utakaowavutia zaidi washiriki kutoka ndani na nje ya nchi.

Mashindano hayo ya siku tatu yaliyofanyika kwenye viwanja vya Klabu ya Gofu ya Gymkhana jijini Arusha yalifanikiwa kuvutia washiriki kutoka vilabu vyote vya mchezo huo hapa nchini sambamba na washiriki wengine kutoka katika mataifa ya Kenya na Uganda. Mchezaji Mercy Nyanchama kutoka nchini Kenya alifanikiwa kuibuka mshindi wa jumla wa mashindano hayo.

Akizungumza kwenye hafla fupi ya kukabidhi zawadi kwa washindi mbalimbali wa mashindano hayo, Meneja Mahusiano wa Benki ya NBC, Bw. Gerald Tarimo pamoja na kuwapongeza washiriki pamoja na washindi mbalimbali wa mashindano hayo alisema benki hiyo itaendelea kuyaunga mkono ikiwemo kuyaboresha zaidi ikiwa ni sehemu ya jitihada zake katika kuchochea ushiriki wa wanawake katika michezo.

MKURUGENZI NBC ATAJA SULUHISHO UIMARISHAJI HUDUMA YA BIMA JUMUISHI NCHINI

Balozi wa Bima Tanzania ambaye pia ni Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Mhandisi Zena Ahmed Saidi (kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Bw Theobald Sabi tuzo maalum baada ya mkurugenzi huyo kuwasilisha mjadala wake kuhusiana na mada: "Bima Jumuishi: Bidhaa Bora na Usambazaji Kupitia Teknolojia," wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Bima mwaka 2024 jijini Dodoma mwishoni mwa wiki. Kilele cha maadhamisho hayo kilihusisha kongamano maalum la wadau mbalimbali wa sekta ya bima nchini, likiongozwa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Bw Theobald Sabi akiwasilisha mjadala wake kuhususiana na mada: "Bima Jumuishi: Bidhaa Bora na Usambazaji Kupitia Teknolojia," wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Bima mwaka 2024 jijini Dodoma mwishoni mwa wiki.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza na wadau mbalimbali wa sekta ya bima nchini wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Bima mwaka 2024 jijini Dodoma mwishoni mwa wiki.
Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Dkt. Baghayo Saqware akizungumza na wadau mbalimbali wa sekta ya bima nchini wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Bima mwaka 2024 jijini Dodoma mwishoni mwa wiki.
Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Bi Khadija Said akizungumza na wadau mbalimbali wa sekta ya bima nchini wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Bima mwaka 2024 jijini Dodoma mwishoni mwa wiki.
Rais wa Taasisi ya Bima Tanzania (IIT) Bi. Magreth Ikongo akizungumza na wadau mbalimbali wa sekta ya bima nchini wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Bima mwaka 2024 jijini Dodoma mwishoni mwa wiki.
Mkuu wa Idara ya Bima, Benki ya NBC Bw Benjamin Nkaka (kulia) akibadilishana mawazo na wadau mbalimbali wa sekta ya bima wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Bima mwaka 2024 jijini Dodoma mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Bw Theobald Sabi (kulia) akijadili jambo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano ya Umma wa benki hiyo Bw Godwin Semunyu wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Bima mwaka 2024 jijini Dodoma mwishoni mwa wiki.

Dodoma, 16 Septemba 2024: Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Bw Theobald Sabi, amesisitiza umuhimu wa teknolojia, elimu kwa umma pamoja na ubia baina ya wadau muhimu wa sekta ya bima ikiwemo serikali, taasisi za fedha na kampuni za mitandao ya simu kama suluhisho muhimu katika kuimarisha na kuchochea kasi ya upatikanaji wa huduma ya bima jumuishi nchini.

Akiwasilisha mjadala wake kuhusiana na mada "Bima Jumuishi: Bidhaa Bora na Usambazaji Kupitia Teknolojia," wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Bima mwaka 2024 jijini Dodoma mwishoni mwa wiki, Sabi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Umoja wa Mabenki Tanzania (TBA) alisisitiza kuhusiana na matokeo ya ukuaji wa teknolojia yanavyoweza kuchochea mabadilliko chanya kwenye sekta hiyo.

Kilele cha maadhamisho hayo kilihusisha kongamano maalum la wadau mbalimbali wa sekta ya bima nchini, likiongozwa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima, sambamba na Kamishna wa Bima Dkt. Baghayo Saqware na Naibu wake Bi Khadija Said pamoja na Balozi wa Bima Tanzania ambaye pia ni Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Mhandisi Zena Ahmed Saidi.

BENKI YA NBC YASHIRIKI MBIO ZA RUANGWA MARATHON 2024

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (katikati walioketi) akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau mbalimbali wakiwemo viongozi waandamizi wa serikali, wasanii maarufu na wadhamini wa mbio za Ruangwa Marathon 2024 zilizofanyika mwishoni mwa wiki katika Uwanja wa Madini wilayani Ruangwa. Benki ya NBC ilikuwa ni moja ya wadhamini muhimu wa mbio hizo.
Meneja wa Kanda ya Pwani wa Benki ya NBC Bi Zubeider Haroun (kushoto) sambamba na maofisa wengine wa benki hiyo akiwemo Meneja wa benki hiyo tawi la Mtwara Bi Editha Mwakatobe (kulia) na Meneja wa benki hiyo tawi la Lindi Bw Iovin Mapunda (katikati) wakishiriki mbio za Ruangwa Marathon 2024 zilizofanyika mwishoni mwa wiki katika Uwanja wa Madini wilayani Ruangwa, zikiongozwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Meneja wa Kanda ya Pwani wa Benki ya NBC Bi Zubeider Haroun (katikati alievaa kofia) akifanya mazoezi ya viungo sambamba na washiriki wengine wa mbio za Ruangwa Marathon 2024 zilizofanyika mwishoni mwa wiki katika Uwanja wa Madini wilayani Ruangwa, zikiongozwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Katika tukio hilo lililovutia washiriki takribani 5,000 wakiwemo viongozi wa serikali, Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel, Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa, na Michezo, Hamiss Mwinjuma, wasanii maarufu na wananchi, Meneja wa Kanda ya Pwani wa Benki ya NBC Bi Zubeider Haroun akiongoza maofisa wengine wa benki hiyo katika kushiriki mbio hizo akiwemo Meneja wa benki hiyo tawi la Mtwara Bi Editha Mwakatobe na Meneja wa benki hiyo tawi la Lindi Bw Iovin Mapunda.
Meneja wa Kanda ya Pwani wa Benki ya NBC Bi Zubeider Haroun (katikati alievaa kofia) sambamba na maofisa wengine wa benki hiyo wakijipongeza na medali zao mara baada ya kushiriki mbio za Ruangwa Marathon 2024 zilizofanyika mwishoni mwa wiki katika Uwanja wa Madini wilayani Ruangwa, zikiongozwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Lindi, Ruangwa: Septemba 16, 2024 - Benki ya Taifa ya Biashara NBC imeshiriki msimu wa pili wa mbio za Ruangwa Marathon 2024 huku ikisisitiza dhamira yake ya kuendelea kuunga mkono jitihada mbalimbali za wadau wa michezo nchini kupitia ushiriki, ufadhili, ubunifu na utoaji wa huduma mbalimbali zikiwemo za kifedha mahususi kwa wadau wa sekta hiyo.

Dhamira ya benki hiyo ni sehemu ya mkakati wake katika kuunga mkono jitihada za serikali na wadau hao katika kukuza vipaji, kujenga afya ya jamii na kuongeza fursa za ajira hususani kwa vijana pamoja kusaidia ufanikishaji wa agenda mbalimbali za kijamii kupitia hamasa ya michezo.

Akizungumza wakati wa mbio hizo zilizofanyika katika Uwanja wa Madini wilayani Ruangwa mwishoni mwa wiki, zikiongozwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Meneja wa Kanda ya Pwani wa Benki ya NBC Bi Zubeider Haroun aliemuwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, alisema nia ya benki hiyo ni kuendelea kuwa mdau mkubwa wa sekta ya michezo nchini sambamba na kutumia vema huduma zake za kifedha katika kuwasaidia wadau wa sekta hiyo muhimu.