Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday 17 September 2024

STANBIC YATOA SH. MIL. 70 KWENYE ZIARA YA BAISKELI YA VODACOM TWENDE BUTIAMA 2024

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Stanbic Tanzania, Manzi Rwegasira, akizungumza wakati wa uzinduzi wa ziara ya waendesha baiskeli kuelekea Butiama 2024, ambayo inadhaminiwa na Vodacom Foundation kwa kushirikiana na Benki ya Stanbic. Uzinduzi huu ulifanyika kama maendesho ya baiskeli ya kijamii "Pedal for Purpose," ambayo ni mwanzo wa ziara hii kuelekea Butiama. Benki ya Stanbic imechangia kiasi cha shilingi milioni 70, ambazo zitatumika kuboresha sekta ya elimu kwa kutoa madawati 1,500; sekta ya afya kwa kuanzisha kliniki zinazozunguka kuhudumia mikoa mbalimbali, na utunzaji wa mazingira kwa kupanda miti 50,000. Kiujumla ziara hii inategemea kuboresha maisha ya watanzania 100,000. Kilele cha ziara hiyo kitafanyika Butiama, Mkoani Mara, tarehe 14 Oktoba.
Mchezaji wa zamani kutoka Nigeria - Nwankwo Kanu (kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania - Philip Besiimire (katikati) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Stanbic Tanzania - Manzi Rwegasira wakifuatilia jambo wakati wa uzinduzi Vodacom Twende Butiama 2024 uliofanyika jijini Dar es salaam.





Mchezaji wa zamani kutoka Nigeria - Nwankwo Kanu (katikati), Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania - Philip Besiimire (kushoto) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Stanbic Tanzania - Manzi Rwegasira (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja.

No comments:

Post a Comment