Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Wednesday, 8 January 2025

CRDB BANK LAUNCHES AFFORDABLE SCHOOL FEES LOANS

The Acting CEO of CRDB Bank, Fredrick Nshekanabo (right), at the launch event of school fees loans for primary & secondary schools. He is flanked by; Head of Personal Banking - Stephen Adili (second right), Head of Business Operations - Feruzi Korongo (second left) as well as the Head of Business at Sanlam Life Tanzania - Kyenekiki Kyando.  

Dar es Salaam: CRDB Bank has launched school fees loans for primary and secondary school students across the country.

The loans, Ada Fasta, loaned through the SimBanking App, are part of CRDB’s ongoing efforts to meet the needs and expectations of its customers, helping them overcome financial challenges.

CRDB Bank Acting Managing Director and CEO, Fredrick Nshekanabo, said yesterday that any parent or guardian can borrow up to 3 Million Tanzania Shillings, which they can repay within six months.

The loan interest rate is only 13 per cent per annum, which is a much lower rate compared to what is available in the market,” Mr. Nshekanabo said.

Mr. Nshekanabo said that the service is being launched at a time when January is traditionally a month filled with significant financial challenges such as school fees, rent and other essential needs, especially after some people have spent substantial when celebrating the year-end holidays.

CRDB, a customer-centric bank, is always designing products and services that meet the needs of its clients, according to Mr. Nshekanabo.

The lender, one of the biggest in the country, for over a decade, introduced and promoted the School Fees Management System, which is now used by over 1,000 schools nationwide.

All parents whose children are in schools using this system—whether they are CRDB customers or not—can benefit from this loan,” Mr. Nshekanabo said.

BENKI YA CRDB YAANZA KUTOA MIKOPO YA ADA SHULE ZA MSINGI, SEKONDARI


Dar es Salaam, 7 Januari 2025: Katika kuukaribisha mwaka mpya 2025, Benki ya CRDB imezindua mikopo ya ada kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari nchini kote. Mikopo hiyo inayoitwa Ada Fasta ni mwendelezo wa juhudi za Benki ya CRDB kukidhi mahitaji na matarajio ya wateja wake ili kuwawezesha kukabiliana na changamoto za kifedha wanazokabiliana nazo.

Akizindua mikopo hiyo inayotolewa kupitia Programu ya SimBanking, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Fredrick Nshekanabo amesema kila mzazi au mlezi mwenye uhitaji anaweza kupata mkopo huo ili kumruhusu mwanafunzi kuendelea na masomo kulingana na ratiba ya muhula husika.

 

Mteja anaweza kukopa mpaka shilingi milioni 3 ambazo atazirudisha ndani ya miezi sita. Riba ya mkopo huu ni asilimia 13 tu kwa mwaka, gharama ndogo zaidi ukilinganisha riba iliyopo sokoni. Nawakaribisha wazazi wote kuitumia fursa hii kuhakikisha watoto wetu wanasoma bila tatizo lolote la ada,” amesema Nshekanabo.

Mkurugenzi huyo amesema wameizindua huduma hiyo kipindi hiki wakitambua kuwa Januari ni mwezi wenye changamoto nyingi za kifedha zinazotokana na mahitaji makubwa yanayokuwepo ikiwamo ada za wanafunzi, kodi ya nyumba na mahitaji mengine muhimu hasa baada ya kila mtu kuwa ametumia kiasi kikubwa cha fedha kusherehekea sikukuu za mwisho wa mwaka.

Ikiwa Benki inayomsikiliza mteja na kumweka mbele katika mikakati ya biashara, amesema wakati wote wanabuni huduma na bidhaa zinazokidhi mahitaji ya wateja na Januari hii wamekuja na jambo jipya mahususi kwa kila mzazi au mlezi wa mwanafunzi nchini.


Zaidi ya muongo mmoja Benki ya CRDB ilizindua nakuutambulisha Mfumo wa Makusanyo ya Ada Shuleni yaani School Fees Management System ambao mpaka sasa unatumiwa na zaidi ya shule 1,000 nchini kote ambazo sasa wanafunzi wake watanufaika na mikopo hii iliyozinduliwa.

Hii ni fursa kwa shule zote binafsi nchini kujiunga na mfumo huu wa makusanyo ya ada ili kutoa fursa kwa wazazi kukopa ada wakati wowote watakapohitaji ili watoto waendelee na masomo yao. Wazazi wote waliopo kwenye shule zinazoutumia mfumo huu wawe ni wateja wetu ama la, wanayo fursa ya kunufaika na mikopo hii,” amesema Nshekanabo.


Mzazi au mlezi atakayeomba mkopo huu, amesema atapata fedha husika zitakazoingizwa kwenye akaunti ya shule moja kwa moja na yeye kupata risiti ya uthibitisho kwamba amelipa ada inayotakiwa kwa ajili ya mtoto wake.

Kwa kuwawezesha wazazi na walezi kulipa ada kwa wakati, Nshekanabo amesema wana imani watakuwa wamesaidia kuboresha elimu kwa kuwawezesha wanafunzi kuhudhuria masomo yao bila vikwazo huku shule zikiweza kujiendesha na kutoa maarifa bora yanayohitajika kwa watoto wa Kitanzania.

Kwa mzazi au mlezi ambaye ameajiriwa na mshahara wake unapitia Benki ya CRDB, anaweza kupata mkopo wa ada kwa kuingia kwenye Programu ya SimBanking kisha akabofya sehemu ya mikopo ambako atatakiwa kuingiza ‘control number’ aliyotumiwa na shule kwa ajili ya malipo ya ada na programu itamwonyesha kiasi cha juu anachoruhusiwa kukopa.


Baada ya hapo, mteja atatakiwa kuingiza kiasi anachokitaka na kupendekeza muda anaotaka kulipa deni hilo ndani ya miezi sita ili kukamilisha maombi yake. Akishafanya hivyo, Benki ya CRDB itaingiza fedha zilizoombwa kwenye akaunti ya shule anakosoma mtoto hivyo kumruhusu asome kwa utulivu.

Ukiacha faida zilizopo kwa pande zote mbili yaani shule na mzazi au mlezi, mfumo wa makusanyo ya ada wa Benki ya CRDB ni rahisi kuutumia kwani mteja anaweza kulipa ada kupitia SimBanking, CRDB Wakala au kutembelea tawi la Benki ya CRDB.

Tuesday, 7 January 2025

POPOTE, KILA MTU NI MSHINDI! WATEJA WA VODACOM WAJAZIWA MAFUTA BURE

Afisa BIMA wa VodaBima kutoka Vodacom Tanzania PLC Kanda ya Ziwa, Hellen Masali akimuwekea mafuta mteja wa kampuni hiyo, Omari Ramadhan jijini Mwanza. Mafuta hayo yametolewa bure ikiwa ni moja ya adhma ya kampeni yao ya msimu wa sikukuu ya kurejesha tabasamu kwa wateja wake katika msimu huu wa sikukuu. Ili kushinda Mafuta bure endelea kulipia kwa kutumia M-Pesa.
Afisa BIMA wa VodaBima kutoka Vodacom Tanzania PLC Kanda ya Ziwa, Hellen Masali akimuwekea mafuta mteja wa kampuni hiyo, Zacharia Regan jijini Mwanza.
Mkuu wa kanda ya ziwa kutoka Vodacom Tanzania PLC, Venance Chapaulinge akimuwekea mafuta mteja wa kampuni hiyo Rajabu Kawambwa jijini Mwanza.


Monday, 6 January 2025

DKT. KIKWETE AKOSHWA NA USHIRIKI WA WADAU BINAFSI KWENYE MIRADI YA MAENDELEO, AIPONGEZA BENKI YA NBC

Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete (wa tatu kulia) akikabidhi tuzo maalum kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw. Theobald Sabi (wa pili kulia) ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wa benki hiyo katika kufanikisha ujenzi Kituo cha Afya cha Kizimkazi kilichopo Wilaya ya Kusini, Unguja wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa kituo hicho iliyofanyika mwishoni mwa wiki Zanzibar. Wanaoshuhudia ni pamoja na Waziri wa Afya Zanzibar Bw. Nassor Ahmed Mazrui (kushoto) na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mahmoud Thabit Kombo (kulia).
Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete (kushoto) pamoja na viongozi wengine waandamizi wa chama na serikali visiwani Zanzibar wakisikiliza taarifa fupi kuhusu Kituo kipya cha Afya cha Kizimkazi kilichopo Wilaya ya Kusini, Unguja kutoka kwa Mwenyekiti wa taasisi ya Samia Foundation ambae pia ndio Mhandisi wa mradi huo, Mhandisi Fatma Kara (alieshika fimbo) wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa kituo hicho iliyofanyika mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw. Theobald Sabi (wa pili kulia). Benki ya NBC ni mmoja wa wadau muhimu kwenye ujenzi wa kituo hicho kilichojengwa kwa ufadhili wa Taasisi ya Samia Foundation.
Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete (wa tatu kushoto) pamoja na viongozi wengine waandamizi wa chama na serikali visiwani Zanzibar wakisikiliza maelezo kuhusu vifaa tiba mbalimbali vilivyopo kwenye Kituo kipya cha Afya cha Kizimkazi kilichopo Wilaya ya Kusini, Unguja kutoka kwa mmoja wa wataalam wa afya kituoni hapo (alieshika mic) wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa kituo hicho iliyofanyika mwishoni mwa wiki.
Ushirikiano na ubia baina ya serikali na wadau mbalimbali ikiwemo taasisi binafsi ni njia rahisi zaidi katika kuchochea kasi ya maendeleo kwa faida ya wananchi. Ushirikiano wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Taasisi ya Samia Foundation, Taasisi ya Ahmed Al Falas Foundation na Benki ya NBC hadi kufanikisha mradi huu ni muendelezo wa mifano mizuri ya kuigwa…hongereni sana,’’ - Dkt. Kikwete.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Bw. Theobald Sabi (pichani) alisema ushiriki wa benki hiyo kwenye mradi huo ni muendelezo wa jitihada zake kupitia sera yake ya Uwajibikaji kwa Jamii (Citizenship), ambapo benki hiyo imeendelea kutenga sehemu ya faida yake kila mwaka ili kusaidia kutatua changamoto mbalimbali katika sekta za afya, elimu, mazingira, elimu ya fedha, na ajira.
Wananchi wakifuatilia uzinduzi huo.

Zanzibar: Januari 4, 2024 -
 Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete amepongeza ushirikiano baina ya wadau binafsi na serikali katika kufanikisha miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ile inayohusiana na afya, akibainisha kuwa hatua hiyo ni chachu muhimu zaidi katika kuchochea kasi ya maendeleo nchini.

Dkt. Kikwete alitoa pongezi hizo mwisho wa wiki wakati akizindua rasmi Kituo cha Afya cha kisasa cha Kizimkazi kilichopo Wilaya ya Kusini, Unguja, Zanzibar kilichojengwa kwa ushirikiano baina ya serikali ya Mapinduzi Zanzibar na wadau mbalimbali hususani Taasisi ya Samia Foundation, Taasisi ya Ahmed Al Falas Foundation na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC).

Hafla fupi ya uzinduzi wa kituo hicho chenye thamani ya sh bil 4.4 ilihudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya afya visiwani Zanzibar akiwemo Waziri wa Afya Zanzibar Bw Nassor Ahmed Mazrui, Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar, Dkt Mngereza Mzee Miraji na viongozi mbalimbali waandamizi wa chama na serikali.

Zaidi, walikuwepo viongozi na maofisa wa taasisi hizo wadau ambapo taasisi ya Samia Foundation iliongozwa na Mwenyekiti wa taasisi hiyo ambae pia ndio Mhandisi wa mradi huo, Mhandisi Fatma Kara, Muwakilishi wa Taasisi ya Ahmed Al Falas Foundation na maofisa wa benki ya NBC wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Bw Theobald Sabi pamoja na wananchi.

Thursday, 2 January 2025

RAIS MWINYI AIPONGEZA NMB KUDHAMINI SHUGHULI MBALIMBALI ZA SERIKALI


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Wawakilishi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, ameipongeza Benki ya NMB kwa kuendelea kuunga mkono shughuli mbalimbali za Serikali yake, ikiwemo Shamrashamra za Miaka 61 za Mapinduzi ya Zanzibar, ilikodhamini na kushiriki Siku ya Kitaifa ya Mazoezi na Michuano ya Kombe la Mapinduzi.


Pongezi hizo amezitoa mapema Jumatano Januari Mosi, wakati Dk. Mwinyi alipoongoza maelfu ya Wazanzibar kushiriki Siku ya Kitaifa ya Mazoezi Zanzibar kwenye Uwanja wa mnazi mmoja wilayani Wete mkoa wa kaskazini Pemba, ambayo ni sehemu tu ya shamrashamra za Miaka 61 ya Mapinduzi ya Matukufu Zanzibar, ambayo kilele chake kitakuwa Januari 12.


Dk. Mwinyi ameipongeza NMB kwa kufadhili mazoezi hayo, ambako ilikabidhi ‘tracksuit’ 100 za kuvaa viongozi, zikiwa na thamani ya Sh. Mil. 9, huku ikidhamini Michuano ya Kombe la Mapinduzi (Mapinduzi Cup 2025) kwa Sh. Mil. 50, mchango uliomsukuma Rais Mwinyi kuiomba taasisi hiyo kudumisha mashirikiano hayo.


Niwashukuru sana Benki ya NMB kwa kuendelea kuunga mkono shughuli mbalimbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) na hata Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wameshiriki pakubwa katika tukio hili muhimu kwa mustakabali wa Afya za Wazanzibar, wameshiriki na kutufanya tupendeze kwa sare walizotoa."


Hongereni sana NMB na kimsingi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, inatambua, inathamini na kujali mchango wenu mkubwa kwa maendeleo na ustawi wa Wazanzibar. SMZ inaamini mtaendelea kushirikiana nayo katika kuharakisha maendeleo ya mtu mmoja mmoja na taifa,” alisema Dk. Mwinyi katika mazoezi hayo.


Naye Meneja wa NMB Kanda ya Zanzibar, Bi. Naima Said Shaame, alisema benki yake imekuwa mshirika mkubwa wa shughuli mbalimbali za Serikali ya Zanzibar na ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiwemo Sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar, inakodhamini kwa miaka 12 sasa.


Huu ni mwaka wa 12 sasa NMB inashirikiana na SMZ kufanikisha Sherehe za Mapinduzi, ambako mwaka huu tumekabidhi ‘tracksuit’ za mazoezi 100 zenye thamani ya Sh. Mil. 9, tukiamini kwamba mchango huo utakuwa chachu ya kuhamasisha mazoezi vizsiwani Zanzibar na Tanzania kwa ujumla wake."


Pia, tumetoa Sh. Mil. 50 kudhamini Kombe la Mapinduzi, udhamini ambao pamoja na ‘tracksuit’ hizo, tunaamini kwamba, ni kilelezo na uthibitisho wa dhati kuwa NMB inathamini michezo, kwani afya zetu zinaimarika zaidi kupitia michezo na uimara wa afya ndio chachu ya kukua kiuchumi kwa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla."

PRESIDENT MWINYI COMMENDS NMB FOR SPONSORING GOVERNMENT INITIATIVES


The President of Zanzibar and Chairman of the House of Representatives, Dr. Hussein Ali Mwinyi, has praised NMB Bank PLC for its ongoing support of various government initiatives, including the 61st Anniversary Celebrations of the Zanzibar Revolution (Mapinduzi). NMB sponsored and participated in the National exercise day as well as the Mapinduzi Cup tournament.


President Mwinyi expressed his gratitude on Wednesday, January 1st, while leading thousands of Zanzibaris in the National Exercise Day at the Mnazi Mmoja grounds in Wete District of North Pemba Region. This event is part of the celebrations marking 61 years of the Zanzibar Revolution, culminating on January 12th.


Dr. Mwinyi commended NMB for funding the exercises and providing 100 tracksuits for leaders, valued at TZS 9 million. The bank also sponsored the Revolution Cup 2025 with TZS 50 million, prompting him to encourage the continued partnership.


"I extend my sincere thanks to NMB Bank for continuously supporting various activities of the Zanzibar Revolutionary Government (SMZ) and even the Government of the United Republic of Tanzania. Their significant participation in this event is crucial for the health of Zanzibaris, and they have enhanced our appearance with the attire provided," Dr. Mwinyi remarked.


He emphasized that the Zanzibar Revolutionary Government recognizes and appreciates NMB's significant contributions to the development and welfare of Zanzibaris, expressing confidence that the cooperation will continue.


NMB's Zanzibar Regional Manager, Ms. Naima Said Shaame, stated that the bank has been a long-time partner of both the Zanzibar government and the United Republic of Tanzania, sponsoring the Revolutionary Celebrations for 12 years.


"This marks the 12th year that NMB has collaborated with the SMZ to facilitate the Revolutionary Celebrations. This year, we have provided 100 exercise tracksuits worth TZS 9 million, believing this contribution will promote exercise in Zanzibar and throughout Tanzania," Ms. Naima explained.


Additionally, Ms. Shaame highlighted the TZS 50 million sponsorship for the Revolution Cup, noting that both the sponsorship and the tracksuits demonstrate NMB's commitment to sports, as they enhance our health which is vital for economic growth.

Tuesday, 31 December 2024

NMB SPONSORS MAPINDUZI CUP 2025 & NATIONAL EXERCISE DAY IN ZANZIBAR


NMB Bank has announced a sponsorship of 50 million Tanzanian shillings for the Zanzibar Mapinduzi Cup 2025, set to commence on January 1, 2025, at Gombani Stadium in Pemba. Unlike previous years, this tournament will feature national teams rather than club teams from Tanzania Mainland and Zanzibar.


In addition to this sponsorship, NMB has also donated 100 tracksuits valued at 9 million shillings to be worn by officials of the Zanzibar Revolution Government on National Exercise Day (January 1, 2025). This event is part of the celebrations for the 61st Anniversary of the Zanzibar Revolution, held under the theme "Peace, Unity, and Solidarity for Our Development - Revolution Forever."


The handover ceremony for the sponsorship dummy cheque and tracksuits took place at the Conference Hall of the Ministry of Information, Youth, Culture, and Sports in Zanzibar whereby NMB's Acting Zanzibar cluster Manager, Ahmed Jumaa Nassor, presented the items to hon. Fatma Hamad Rajabu, the Permanent Secretary of the Ministry, in the presence of NMB Zanzibar's Government Business Relationship Manager, Jaha Khamisi.


During her remarks upon receiving the cheque and tracksuits, Fatma expressed gratitude to NMB for their contribution, cooperation, and solidarity with the government led by President Dr. Hussein Ali Mwinyi. She urged the bank to continue this partnership for the prosperity and development of Zanzibar and its people.

"NMB's involvement is not just during the Zanzibar Revolution celebrations; they are at the forefront of promoting the development of the islands and their residents in many areas, including sports. They have been a consistent sponsor of the Mapinduzi Cup for several years, helping to increase employment through sports," she noted.

NMB YADHAMINI KOMBE LA MAPINDUZI 2025, YAFADHILI SIKU YA MAZOEZI KITAIFA ZANZIBAR


Benki ya NMB, imetangaza udhamini wa Shilingi Milioni 50 wa michuano ya Kombe la Mapinduzi ya Zanzibar (Mapinduzi Cup 2025), inayotarajia kuanza Januari 03, 2025 kwenye Uwanja wa Gombani visiwani Pemba, ambayo itashirikisha timu za Taifa, badala ya klabu za Tanzania Bara na Zanzibar kama ilivyozoeleka.


Sambamba na udhamini huo, NMB pia imekabidhi 'tracksuit' 100 zenye thamani ya Shilingi Milioni 9 za kuvaa viongozi wa Serikali ya Zanzibar katika Siku ya Kitaifa ya Mazoezi (Januari 1, 2025), ambayo ni sehemu ya Shamrashamra za Miaka 61 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, ambayo inafanyika chini ya kaulimbiu: 'Amani, Umoja na Mshikamano kwa Maendeleo Yetu - Mapinduzi Daima.'


Hafla ya makabidhiano ya hundi ya udhamini na 'tracksuit' hizo, imefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Zanzibar, ambako Kaimu Meneja wa NMB Kanda ya Zanzibar, Ahmed Jumaa Nassor, alimkabidhi Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bi. Fatma Hamad Rajabu, mbele ya Meneja Uhusiano wa NMB Zanzibar, Jaha Khamisi.


Akizungumza wakati wa hafla hiyo baada ya kupokea hundi, Bi. Fatma aliishukuru NMB kwa mchango wao, ushirikiano na umoja wanaoonesha kwa Serikali ya Zanzibar inayoongozwa na Rais Dk. Hussein Ali Mwinyi, na kuitaka kudumisha mashirikiano hayo kwa ustawi wa Zanzibar na maendeleo ya Wazanzibar kwa ujumla.


Alibainisha kuwa mchango na ushiriki wa NMB sio tu katika Sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar, bali iko mstari wa mbele daima kuchagiza maendeleo ya visiwa hivyo na wakazi wake na katika nyanja nyingi, ikiwemo michezo, ambako imejitoa vya kutosha kudhamini Kombe la Mapinduzi kwa miaka kadhaa na kuchangia ongezeko la ajira kupitia michezo.

"Wazanzibar wengi wanahudumiwa na NMB na uwingi wao unalenga kuiwezesha benki kukuza pato lao ili nao wanufaike na mchango wa maendeleo ya Zanzibar na watu wake. Tunawapongeza kwa kufadhili Siku ya Mazoezi Kitaifa, lakini pia kwa udhamini wenu mnono katika Kombe la Mapinduzi 2025."

100 NMB CUSTOMERS WIN 10M/- CASH PRIZES IN ‘MASTABATA LA KIBABE’ 7th DRAW


One hundred lucky NMB Bank customers won 100,000/- cash prizes each during the 7th draw of the MastaBata la Kibabe' campaign held at the bank’s Tegeta branch in Dar es Salaam region recently.


The three months MastaBata la Kibabe campaign unveiled in November this year seeks to encourage consumers to make use of NMB Mastercard at Point of Sales (PoS) machines, online and QR link payments.


Speaking during the draw, the NMB Tegata Branch Manager Margret Lwiva said the bank’s rewards campaign not only seeks to promote financial inclusion but also compliments the country’s cashless economy agenda.


"This three campaign seeks to enhance the transition from cash to digital payments as it has proved more secure, convenient, and user-friendly.” Lwiva said.


Lwiva urged that the campaign is part of the bank’s commitment to reward customers for their loyalty.


"During this three-month campaign, lucky customers will win cash prizes of up to 300m/-. Up to today, we have already dished out 76.4m/- to 712 lucky winners,” she stressed.


She added that the bank has also dished out shopping vouchers to 222 customers, cash prizes of up to 500,000/- during the campaign's monthly draws.


She added that the bank’s campaign also seeks to boost domestic tourism where lucky winners will get fully paid trips to some of the country’s unique attractions.


During this campaign there will be 10 winners in the domestic tourism category, with five lucky individuals earning the chance to visit Mikumi National Park and the other five set to explore the Ngorongoro Conservation Area.


She added, “In addition, 10 lucky winners will each receive school fees worth 4m/- each ensuring they do not worry when schools reopen in January next year.