Blog Rebranding Teaser_030826

Blog Rebranding Teaser_030826

Absa Banner_211026

Stanbic Bank Banner_201026

Wednesday, 21 October 2026

WAZIRI KAPINGA ASIFU INSTAPRENYUA YA CRDB KWA KUCHOCHEA UKUAJI WA UCHUMI WA KIDIJITALI

Dar es Salaam; Oktoba 21, 2026 - Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga, ameipongeza Benki ya CRDB kwa kuendelea kuwa mstari wa mbele katika kuwawezesha wajasiriamali kupitia teknolojia, ubunifu na upatikanaji wa mitaji, akisema juhudi hizo zinachangia kujenga mazingira wezeshi ya biashara na kukuza uchumi shindani unaoendana na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Waziri Kapinga aliyasema hayo Oktoba 21, 2026, wakati akifungua msimu wa nne wa Jukwaa la Instaprenyua 2026 lililofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Mlimani City jijini Dar es Salaam. Aliwahimiza wajasiriamali kutumia fursa zinazotokana na uchumi wa kidijitali kupanua masoko, kuongeza ufanisi na kukuza biashara zao.

Alisema Serikali inaendelea kuweka mazingira rafiki kwa sekta binafsi kustawi, huku ikitambua mchango wa wajasiriamali katika kukuza shughuli za kiuchumi, kuongeza ajira na kuimarisha ushindani wa biashara nchini.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Musa Kitambi, alisema Jukwaa la Instaprenyua ni sehemu ya mkakati wa benki hiyo wa kujenga uhusiano wa karibu na wajasiriamali, kuelewa changamoto zinazowakabili na kuwaunganisha na maarifa, mitaji na suluhisho za kifedha zinazochochea ukuaji wa biashara zao.

Jukwaa la Instaprenyua 2026 linafanyika kwa siku mbili, Oktoba 21 na 22, chini ya kaulimbiu ya “Smartisha Biashara.” Linajumuisha mijadala, mafunzo, maonesho na majadiliano ya kibiashara yanayofanyika kupitia Deal Rooms, yakilenga kuwawezesha wajasiriamali kupata maarifa mapya, kujenga mitandao ya kibiashara na kutambua fursa za kukuza biashara zao.

Katika jukwaa hilo, Benki ya CRDB imejipanga kutoa huduma mbalimbali kwa wajasiriamali, zikiwemo ufunguzi wa akaunti, huduma za mikopo, bima za biashara na kuwaunganisha na suluhisho za kidijitali kama CRDB Lipa Hapa, SimBanking na Internet Banking.

Kupitia huduma hizo na jukwaa la Instaprenyua, CRDB inaendelea kusisitiza umuhimu wa kuunganisha upatikanaji wa huduma za kifedha na matumizi ya teknolojia ili kuwawezesha wajasiriamali kuimarisha shughuli zao, kupanua wigo wa masoko na kutumia fursa zinazotokana na uchumi wa kidijitali.


Fuata Kitomari Banking & Finance Blog kwa habari, uchambuzi na taarifa za hivi karibuni kuhusu sekta ya benki, biashara na fedha.

Mitandao ya kijamii:








No comments:

Post a Comment