Blog Rebranding Teaser_030826

Blog Rebranding Teaser_030826

Absa Banner_170926

Absa Banner_170926

Stanbic Bank Banner_070826

Stanbic Bank Banner_070826

Friday, 18 September 2026

NYOTA BIGI MSIMU WA PILI YARUDI TENA: SERENGETI LITE NA KUNTA AFRICA WATAFUTA NYOTA MPYA MKUBWA NCHINI TANZANIA

DAR ES SALAAM, TANZANIA – 17 Septemba 2026: Je, umewahi kujikuta ukifanya kazi ambayo unajua kabisa siyo kwa ajili yako? Au kujiuliza kama kile unachokifanya kwa kujifurahisha ukiwa nyumbani, njiani au wakati wako wa mapumziko kinaweza kuwa zaidi ya burudani?

Serengeti Lite, kinywaji kutoka Kampuni ya Vinywaji ya Serengeti, kwa kushirikiana na KUNTA Africa, wamezindua rasmi Nyota Bigi Msimu wa Pili, mpango unaolenga kusaka na kukuza nyota mpya wa Tanzania wenye vipaji mbalimbali vya ubunifu.

Katika msimu huu, usaili utafanyika katika mikoa minne ya Dar es Salaam, Mwanza, Arusha na Dodoma, ambapo safari ya kusaka vipaji itaanza jijini Dar es Salaam tarehe 3 Oktoba 2026, ikifuatiwa na Mwanza tarehe 10 Oktoba, Arusha tarehe 17 Oktoba, na Dodoma tarehe 24 Oktoba 2026.

Nyota Bigi Msimu wa Pili unalenga kuwafikia waimbaji, wacheza muziki, waigizaji, wachekeshaji, wabunifu, wanamitindo pamoja na wenye vipaji vingine vya ubunifu ambavyo bado havijagunduliwa na kupata nafasi ya kuonekana hadharani.

Mpango huo ni sehemu ya kampeni ya Serengeti Lite inayojulikana kama “Lite Your Imagination”, inayolenga kuwahamasisha vijana kuchukulia ubunifu wao kwa uzito, kujieleza na kutambua uwezo wa vipaji vyao katika kujenga maisha na fursa za kiuchumi.

Jukwaa la kugundua vipaji vipya

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Nyota Bigi Msimu wa Pili jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Masoko na Ubunifu wa Kampuni ya Vinywaji ya Serengeti, Henry Esiaba, alisema jukwaa hilo limeanzishwa kwa kutambua kuwa vipaji vipo kila mahali na kinachohitajika ni fursa ya kuvionyesha.

“Tuna vipaji vingi katika kila kona ya nchi hii. Ila kinachokosekana wakati mwingine ni nafasi ya kuonekana. Nyota Bigi ipo kwa ajili ya kuwapa vijana wa Tanzania jukwaa hilo. Tumerudi kwa msimu wa pili, pamoja na washirika wetu KUNTA Africa, kwa sababu tunataka kugundua vipaji zaidi, kuviweka mbele ya hadhira kubwa na kuvipa msukumo unaostahili, popote vilipo,” alisema Esiaba.

Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Bia wa Kampuni ya Vinywaji ya Serengeti, Rhona Namanya, alisema msimu wa pili umefanyiwa maboresho na kupanuliwa zaidi kwa kufikisha programu hiyo katika miji mingine ya Tanzania, tofauti na msimu wa kwanza uliolenga zaidi Dar es Salaam.

“Mwaka huu tunafurahi kuwajulisha Watanzania kuwa msimu wa pili utakwenda katika miji mbalimbali Tanzania, ukilinganisha na mwaka jana ambapo tulitafuta vipaji hapa Dar es Salaam tu. Msimu huu wa pili tutakwenda kwenye miji mingine ikiwepo Arusha, Mwanza na Dodoma. Hii inaonyesha dhamira yetu ya kukuza vipaji zaidi hapa Tanzania,” alisema Rhona.

Usajili umefunguliwa

Usajili kwa ajili ya Nyota Bigi Msimu wa Pili tayari umefunguliwa kupitia msimbo wa QR wa Nyota Bigi, tovuti ya Nyota Bigi, WhatsApp au simu.

Waombaji wanatakiwa kuwa na umri wa miaka 18 hadi 35, kuwa na kitambulisho halali na kuwasilisha video fupi inayoonyesha kipaji chao.

Usaili utafanyika ana kwa ana na mtandaoni, hatua inayolenga kutoa fursa kwa wenye vipaji kutoka maeneo mbalimbali kushiriki bila kujali walipo.

Fursa zaidi ya mashindano

Kwa watakaofanikiwa kuvuka hatua za usaili, Nyota Bigi inalenga kuwa daraja la kuwaunganisha washiriki na fursa mbalimbali ndani ya tasnia ya ubunifu na burudani.

Fursa hizo zinaweza kujumuisha kuunganishwa na masoko kupitia mitandao ya kijamii, uanamitindo, burudani, usimamizi wa vipaji pamoja na studio za kurekodi.

Kwa Serengeti Lite, Nyota Bigi inaweka kaulimbiu ya “Lite Your Imagination” katika vitendo kwa kuwapa vijana nafasi ya kugeuza mawazo na vipaji vyao kuwa fursa halisi.

Msimu wa pili wa Nyota Bigi unaendeleza dhamira ya Serengeti Lite ya kusaidia kukuza ubunifu wa vijana nchini Tanzania na kuhakikisha vipaji vinavyopatikana katika maeneo mbalimbali vinapata nafasi ya kuonekana, kuendelezwa na kufikia hadhira pana.

No comments:

Post a Comment