| Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi (aliyekaa katikati), Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga (aliyekaa kushoto), na Mkurugenzi Mkuu wa TANTRADE, Latifa Khamis (aliyekaa kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa kampuni mbalimbali, akiwemo Mkuu wa Kanda ya Dar es Salaam na Pwani wa Vodacom Tanzania Plc, Happiness Shuma (aliyevaa tisheti nyekundu), muda mfupi baada ya kufungwa kwa Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (SABASABA). Vodacom Tanzania Plc ilitambuliwa kama mshirika muhimu wa maonesho hayo baada ya kupewa tuzo mbili; Tuzo ya Nafasi ya Tatu kwa Mshindi wa Jumla wa Maonesho na Tuzo ya Nafasi ya Pili ya Udhamini, ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wake katika kufanikisha maonesho hayo. |
No comments:
Post a Comment