Foreign Exchange Rates

CRDB Bank Advert_070325

Selcom Pesa Advert_110225

Selcom Pesa Advert_110225

Standard Chartered Advert_300125

Standard Chartered Advert_300125

Wednesday, 7 January 2026

WAKAZI WA LINDI WAENDELEA KUSHEREHEKEA MWAKA MPYA NA MAKAPU YA VODACOM

LINDI: Wakazi wa Mkoa wa Lindi wameendelea kuupokea Mwaka Mpya kwa furaha, baada ya kampuni ya Vodacom Tanzania kuendeleza kampeni yake ya kugawa makapu ya sikukuu kwa wateja na wananchi, ikiwa ni sehemu ya kusherehekea mwanzo wa mwaka mpya pamoja na jamii.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Meneja Mauzo wa Vodacom Tanzania Mkoa wa Lindi, Omary Kilumanga, alisema kampeni hiyo inalenga kuwashukuru wateja kwa uaminifu wao, sambamba na kuimarisha uhusiano kati ya kampuni na jamii inayohudumiwa.

Vodacom inaamini katika kushirikiana na wateja wake si tu kupitia huduma za mawasiliano, bali pia katika nyakati za sherehe kama hizi za kuanza mwaka mpya. Tunafurahi kusherehekea pamoja na wakazi wa Lindi,” alisema Kilumanga.

Katika hafla hiyo, Kilumanga (kushoto) aliungana na Afisa wa Vodacom, Feruzi Mlaponi (kulia), kukabidhi makapu ya sikukuu kwa wateja mbalimbali, akiwemo Bi. Anna Milanzi (katikati), hatua iliyopokelewa kwa shukrani na furaha kubwa kutoka kwa wanufaika.

Kwa upande wake, Afisa wa Vodacom Feruzi Mlaponi (kulia) pia alionekana akikabidhi kapu la Vodacom kwa mteja wa kampuni hiyo, Said Kikotokeki (kushoto), akisisitiza kuwa kampeni hiyo ni sehemu ya dhamira ya Vodacom ya kuendelea kuwa karibu na wateja wake katika mikoa yote nchini.

Kampeni ya kugawa makapu ya sikukuu imekuwa ikiendelea katika mikoa mbalimbali hapa nchini, ikiwa ni mkakati wa Vodacom wa kuimarisha mshikamano, kuthamini wateja, na kusherehekea mafanikio ya pamoja katika kuanza mwaka mpya.

Hafla hiyo imefanyika mwishoni mwa wiki mjini Lindi, na imeacha taswira chanya ya ushirikiano kati ya Vodacom na jamii, huku wananchi wakieleza kufurahishwa na hatua hiyo kama ishara ya kujali na kuthamini wateja.

No comments:

Post a Comment