Foreign Exchange Rates

CRDB Bank Advert_070325

Wednesday, 28 January 2026

RAIS SAMIA APONGEZA JUHUDI ZA KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI KATIKA UTUNZAJI WA MAZINGIRA

Dar es Salaam, Tanzania – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameipongeza na kuipatia tuzo Kampuni ya Bia ya Serengeti (Serengeti Breweries Limited – SBL) kwa mchango wake mkubwa katika uhifadhi wa mazingira na kuunga mkono maendeleo endelevu ya taifa.

Tuzo hiyo ya kihistoria ya Pongezi, ambayo ni ya kwanza kutolewa kwa SBL na Kiongozi Mkuu wa Nchi, inaakisi dhamira thabiti ya kampuni hiyo katika kutekeleza mikakati ya Mazingira, Jamii na Utawala Bora (ESG), sambamba na ajenda ya Taifa ya maendeleo endelevu.

Kupitia programu na miradi yake mbalimbali ya kijamii na kimazingira, SBL imeendelea kutoa mchango chanya kwa jamii na mazingira. Hadi sasa, kampuni hiyo imefanikiwa:

  • Kupanda miti zaidi ya 10,000 katika Kanda ya Kaskazini na Kanda ya Kati
  • Kutekeleza miradi ya maji safi na salama zaidi ya 28 kwa jamii zinazozunguka maeneo yake ya uzalishaji
  • Kuwekeza katika kilimo endelevu kwa kuwaunga mkono vijana zaidi ya 300 kupitia mpango wa Kilimo Viwanda

Aidha, SBL imeanzisha mpango wa “Shamba ni Mali”, unaolenga kuwawezesha wakulima kwa kuwapatia mbolea, mbegu bora, teknolojia ya kisasa pamoja na elimu ya kilimo. Kupitia mpango huo, kampuni inalenga kuwafikia wakulima zaidi ya 4,000 ifikapo mwaka 2030, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha uzalishaji wa kilimo na ustawi wa wakulima nchini.

Utambuzi huu kutoka kwa Rais Samia Suluhu Hassan unaonesha nafasi ya SBL kama mdau muhimu katika uhifadhi wa mazingira, maendeleo ya jamii na uendelevu wa kiuchumi, huku ikiendelea kushirikiana na Serikali pamoja na wadau wengine katika kulijenga taifa lenye ustawi wa muda mrefu.

No comments:

Post a Comment