Katika kuendeleza kampeni yake ya kusherehekea msimu wa sikukuu na wateja wake, Vodacom Tanzania Plc imeendelea kugawa makapu maalum ya sikukuu katika maeneo mbalimbali nchini, ikiwa ni njia ya kuonesha shukrani na kuthamini uaminifu wa wateja wake.
Huko Ipinda–Kyela, jijini Mbeya, kampuni hiyo iliendelea na zoezi hilo kwa kushirikiana moja kwa moja na wateja wanaotumia huduma zake kila siku.
Katika tukio hilo, Meneja Mauzo wa Vodacom Tanzania mkoa wa Iringa, Zidiel Mbwambo, alikabidhi Kapu la Sikukuu kwa Rehema Robert Mwang'onda, kama ishara ya kuungana na wateja kusherehekea msimu huu wa furaha. Utoaji huo ulipokelewa kwa shangwe na furaha, huku Rehema akipongeza kampuni kwa kuwa karibu na wateja wake na kuonesha moyo wa kujali katika kipindi hiki cha sikukuu.
Katika tukio jingine lililofanyika katika eneo hilo hilo la Ipinda–Kyela, Ofisa wa M-Pesa kutoka Vodacom Tanzania Plc, Evelyn Mwinuka, naye alikabidhi Kapu la Sikukuu kwa mteja Lukas Njabeki Chuma. Kitendo hicho ni sehemu ya muendelezo wa kampeni ya kampuni hiyo yenye lengo la kurudisha shukrani kwa wateja wanaoendelea kuiamini Vodacom na huduma zake, hususan M-Pesa, kama sehemu muhimu ya maisha yao ya kila siku.
Kupitia kampeni hii, Vodacom inaendelea kuthibitisha dhamira yake ya kuboresha maisha ya wateja, kuwa karibu nao na kushirikiana nao katika misimu muhimu kama hii ya sikukuu. Kampuni imesisitiza kuwa zoezi la ugawaji wa makapu litaendelea katika maeneo mbalimbali nchini, likilenga kugusa maisha ya wateja wengi zaidi.



.jpeg)
No comments:
Post a Comment