Dar es Salaam, Tanzania – Oktoba 2025 – Wadau wa teknolojia jijini Dar es Salaam wamepata nafasi ya kutambulishwa kwa simu mpya ya Redmi 15C kutoka kampuni ya Xiaomi, katika kikao kilicholenga kuonesha uwezo na mwelekeo wa kifaa hicho sokoni.
Tukio hilo, lililofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam, liliwahusisha washiriki katika maonyesho ya karibu ya vipengele vipya vya Redmi 15C, sambamba na bidhaa nyingine ikiwemo Redmi Pad. Pia, washiriki walihamasishwa kujadili mustakabali wa matumizi ya teknolojia janjanja nchini.
Baadhi ya washiriki walipata zawadi mbalimbali kama ishara ya shukrani kwa kushiriki katika utambulisho huo, huku kampuni ya Xiaomi ikisisitiza dhamira yake ya kuendeleza uwepo wake na ushirikiano na watumiaji wa Tanzania.
Waandaaji wa tukio walisema kuwa hafla hiyo iliandaliwa mahsusi kwa wadau ili kuonesha jinsi Redmi 15C inavyoweza kuendana na mahitaji ya jamii ya sasa, inayojikita zaidi katika mawasiliano na matumizi ya kidijitali.



No comments:
Post a Comment