Dar es Salaam, Tanzania:
Vodacom Tanzania PLC imeonesha kwa mara nyingine dhamira yake ya kuwawezesha wanawake na vijana kupitia michezo kwa kudhamini Ligi ya Mpira wa Kikapu ya Dar es Salaam (BDL) 2025, ambayo ilihitimishwa kwa fainali zenye msisimko katika viwanja vya Don Bosco Oysterbay.
Kwa upande wa wanawake, timu ya DB Lioness imetangazwa mabingwa wa ligi hiyo, hatua inayodhihirisha ukuaji wa michezo ya wanawake nchini Tanzania. Ushindi huo unaonyesha fursa zinazozidi kufunguka kwa wachezaji wanawake na mchango wa Vodacom katika kuendeleza usawa wa kijinsia pamoja na michezo nchini.
Kwa upande wa wanaume, timu ya Dar City Basketball iliibuka mabingwa, huku mchezaji Amini Juma akikabidhiwa mfano wa hundi ya shilingi milioni 10 kutoka kwa Mkurugenzi wa Tehama wa Vodacom Tanzania PLC, Bw. Athumani Mlinga. Mchango huo ni sehemu ya mpango mpana wa Vodacom wa uwezeshaji vijana unaolenga kukuza vipaji, kuhamasisha ushiriki wa vijana katika michezo, na kuendeleza mpira wa kikapu nchini.
Tukio hilo lililofanyika mwishoni mwa wiki, lilihudhuriwa na wafanyakazi wa Vodacom, viongozi wa mchezo wa mpira wa kikapu pamoja na mashabiki wengi. Hafla hiyo imeonyesha mshikamano wa michezo na nafasi muhimu ya Vodacom kama mdau mkubwa katika kukuza mustakabali wa michezo nchini Tanzania.


.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)
No comments:
Post a Comment