Dar es Salaam, 7 Oktoba 2025:
Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania PLC wameshiriki kikamilifu katika zoezi la uchangiaji damu lililofanyika katika ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama (NBTS), makao makuu ya Kanda ya Mashariki yaliyopo Ilala, jijini Dar es Salaam.
Shughuli hiyo, ambayo ilikuwa sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja, ilisheheni hamasa kubwa na ushirikiano kutoka kwa wafanyakazi wa Vodacom pamoja na maafisa wa uhamasishaji kutoka NBTS waliokuwa wakisimamia zoezi hilo.
Kupitia tukio hili, Vodacom Tanzania imesisitiza dhamira yake ya kuendelea kushirikiana na jamii na kuhamasisha watanzania kushiriki katika shughuli zenye lengo la kuboresha afya na maisha ya wananchi.
“Kusaidia wengine ni kiini cha huduma bora kwa wateja na jamii kwa ujumla. Zoezi kama hili linaonyesha kuwa huduma kwa wateja sio tu kuhusu biashara, bali pia ni kuhusu kugusa maisha ya watu,” imeelezwa na mwakilishi wa Vodacom wakati wa zoezi hilo.
Kwa Vodacom, Wiki ya Huduma kwa Wateja ni fursa ya kuthibitisha kwa vitendo kuwa huduma bora huenda sambamba na uwajibikaji kwa jamii — kuhakikisha maisha bora, afya njema, na ushirikiano endelevu.







No comments:
Post a Comment