DUBAI, UAE
Benki ya NMB imepokea tuzo maalum kwa kutambuliwa kama benki ya kwanza katika Afrika Mashariki kubuni na kutoa kadi maalum iliyotengenezwa mahsusi kwa ajili ya wajasiriamali wadogo na wa kati (SMEs).
Tuzo hiyo ilikabidhiwa jijini Dubai kwa Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB, Bw. Filbert Mponzi, na Makamu wa Rais wa Malipo wa Mastercard, Bi. Prakrithi Singh, katika hafla ya kitaifa ya utoaji tuzo.
Hafla hiyo ilihudhuriwa pia na viongozi wengine wa NMB akiwemo Mkuu wa Idara ya Biashara, Bw. Alex Mgeni, na Meneja Mwandamizi wa Idara ya Kadi, Bw. Manfred Kayala.

.jpeg)

No comments:
Post a Comment