Dar es Salaam, Tanzania – Jumanne, 23 Septemba 2025 – Watanzania wanaolipa ada za shule, kujaza mafuta, kufanya manunuzi ya nyumbani au kununua vocha za simu kupitia njia za kidijitali za Benki ya Stanbic sasa watapata fursa ya kipekee. Kupitia kampeni mpya ya “Masta wa Miamala”, Benki ya Stanbic Tanzania itawazawadia wateja kwa miamala ya kila siku inayotumika kwenye maisha yao.
Kampeni hii ya miezi mitatu inalenga kuongeza matumizi ya njia mbalimbali za Stanbic kuanzia kadi za Visa, ATM, mtandao wa Smart App wenye zaidi ya mawakala 600, benki mtandaoni (Internet Banking) na USSD 15029#. Lengo ni si tu kukuza matumizi ya kidijitali, bali pia kuwahamasisha wateja wasiotumia akaunti zao na kuwapa nafasi ya kufurahia urahisi na usalama wa miamala isiyo na fedha taslimu.
Kupitia mpangilio wa zawadi, wateja watanufaika katika ngazi tofauti:
- Watumiaji wakubwa: Zawadi hadi TZS 100,000
- Watumiaji wa kati: Zawadi ya TZS 50,000
- Akaunti zisizotumika: Hamasa ya TZS 25,000
- Bonasi za papo hapo: Hadi TZS 300 kwa kila muamala
Kauli za Viongozi
Emmanuel Mahodanga, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi, alisema:
“Kuhifadhi fedha benki huwa bora zaidi pale unaporahisisha maisha ya kila siku. Masta wa Miamala ni njia yetu ya kuonyesha kuwa huduma za kidijitali sio tu salama na rahisi, bali pia zenye manufaa. Tunaposherehekea miaka 30 nchini Tanzania, kampeni hii inaonyesha dhamira yetu ya kudumu ya kutembea na wateja wetu na kuchangia katika safari ya ukuaji wa taifa.”
Avin Ngoo, Meneja wa Idara ya Mawakala, alisisitiza umuhimu wa mawakala:
“Kupitia mtandao wa mawakala, Stanbic inavunja vizuizi vya umbali na gharama kwa kusogeza huduma za kifedha karibu na kila jamii. Kila muamala, hata ule mdogo, ni ishara kwamba wateja wetu ni sehemu ya familia ya Stanbic.”
Shabani Mwenda, Kaimu Mkuu wa Uboreshaji wa Huduma Binafsi, aliongeza:
“Kufanya miamala kidijitali siyo suala la urahisi pekee, bali ni ujumuishi. Iwe ni kupitia kadi, App, USSD au benki mtandaoni, kila muamala una thamani na unaisaidia Tanzania kusogea mbele kuelekea mfumo wa kifedha salama na wenye uwazi zaidi.”
Irene Mutabihirwa, Meneja wa Uimarishaji wa Mahusiano ya Wateja, alisema:
“Kadi zinawapa wateja wetu zaidi ya urahisi wa malipo. Zinatoa usalama, kumbukumbu za kifedha na kujiamini. Kila unapotumia kadi yako, unasogea karibu na mustakabali salama na wa kidijitali.”
Zaidi ya Promosheni ya Kawaida
Kampeni hii siyo promosheni ya kawaida. Itapanua wigo wake zaidi ya njia za benki na kufika kwenye maeneo ya kila siku ya Watanzania. Watu mashuhuri wataungana na Stanbic kuwaibukia washindi kwenye maduka makubwa, vituo vya mafuta na maeneo mengine ya umma, wakibadilisha miamala kuwa matukio ya kijamii yanayoonyesha athari chanya ya kampeni hii.
Taarifa za washindi pia zitashirikishwa kwenye majukwaa ya kidijitali, zikionyesha namna tabia za kawaida za kifedha zinavyoweza kuleta zawadi halisi.
Kampeni hii pia inaonyesha kukua kwa matumizi ya malipo ya kidijitali nchini. Kadri Watanzania wengi wanavyochagua njia salama zisizo na pesa taslimu, Masta wa Miamala inathibitisha nafasi ya uongozi wa Stanbic katika kujenga uaminifu, urahisi na upatikanaji kwenye mfumo wa kifedha wa taifa.
Stanbic inaposherehekea miaka 30 nchini Tanzania, benki inasisitiza kuwa kampeni hii ni sehemu ya dhamira yake pana ya kusaidia familia, biashara na jamii, huku ikijenga sekta ya kifedha ya kisasa na jumuishi inayochangia maendeleo ya taifa.
Mawasiliano kwa Vyombo vya Habari
Jina: Dickson Senzi
Cheo: Meneja Mwandamizi wa Uhusiano na Mawasiliano
Barua pepe: Dickson.Senzi@stanbic.co.tz
Kuhusu Benki ya Stanbic Tanzania
Benki ya Stanbic Tanzania ni mtoa huduma mkubwa wa kifedha, ikitoa suluhisho mbalimbali kwa wateja binafsi, biashara na taasisi. Kwa kuzingatia uwekezaji endelevu na ushirikiano wa kimkakati, benki hii inachukua nafasi muhimu katika kuunga mkono maendeleo ya kiuchumi ya Tanzania na ushirikiano wa kikanda.
Stanbic Bank ni sehemu ya Standard Bank Group, benki kubwa zaidi barani Afrika kwa mali, yenye uwepo katika nchi 20 kote barani. Kupitia mtandao huu, benki inaunganisha Tanzania na ukuaji wa Afrika na masoko ya kifedha duniani.

No comments:
Post a Comment