Foreign Exchange Rates

CRDB Bank Advert_070325

Selcom Pesa Advert_110225

Selcom Pesa Advert_110225

Standard Chartered Advert_300125

Standard Chartered Advert_300125

Friday, 19 September 2025

VODACOM YAZINDUA OFISI YA KANDA YA KASKAZINI PAMOJA NA DUKA JIPYA JIJINI ARUSHA

Mkuu wa Kanda ya Kaskazini wa Vodacom Tanzania PLC, Bw. George Venanty, akizungumza wakati wa uzinduzi wa ofisi mpya ya Kanda ya Kaskazini jijini Arusha. Tukio hilo lilihudhuriwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Philip Besiimire, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa kampuni hiyo, David Tarimo, pamoja na wafanyakazi wengine wa Vodacom Tanzania PLC.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Philip Besiimire, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa kampuni hiyo, David Tarimo, na Mkurugenzi wa Biashara, Brigita Shirima, wakiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wengine wa Vodacom wakati wa uzinduzi wa ofisi ya Kanda ya Kaskazini pamoja na duka jipya la Vodacom jijini Arusha.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Vodacom Tanzania PLC, David Tarimo (wa pili kushoto), akimsikiliza Meneja wa Maduka ya Rejareja wa kampuni hiyo, Vanessa Mlawi, akielezea huduma mbalimbali za kidijitali wakati wa uzinduzi wa duka jipya pamoja na ofisi ya Vodacom Kanda ya Kaskazini zilizoko katika jengo la PAPU jijini Arusha. Uzinduzi huo, uliofanyika kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 25 ya kampuni hiyo, unaendelea kusogeza huduma karibu na wateja kupitia njia mbalimbali, ikiwemo za kidijitali. Kulia (mwenye kofia nyekundu) ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Vodacom, Philip Besiimire.
Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya uzinduzi wa ofisi ya Kanda ya Kaskazini na duka jipya lililoko katika jengo la PAPU jijini Arusha.
Wateja wa muda mrefu wa Vodacom Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kupokea zawadi kama ishara ya shukrani kwa uaminifu wao kwa kampuni hiyo kwa kipindi cha miaka 25. Tukio hilo limefanyika jijini Arusha kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 25 ya kampuni hiyo.

No comments:

Post a Comment