Foreign Exchange Rates

CRDB Bank Advert_070325

Selcom Pesa Advert_110225

Selcom Pesa Advert_110225

Standard Chartered Advert_300125

Standard Chartered Advert_300125

Thursday, 21 August 2025

NMB YABORESHA UHUSIANO NA WATEJA WA BIASHARA KUPITIA NMB BUSINESS CLUB – DODOMA

Dodoma – Benki ya NMB imeendelea kuimarisha uhusiano wake na wateja wa kibiashara kwa kutoa elimu na ufafanuzi kuhusu huduma na masuluhisho mbalimbali ya kifedha kupitia NMB Business Club, iliyoandaliwa jijini Dodoma jana.

Meneja Mwandamizi wa Idara ya Biashara Makao Makuu ya NMB, Reynold Tony, alisema benki hiyo ina dhamira ya kuhakikisha wafanyabiashara wanapata uelewa mpana juu ya bidhaa na mipango ya kifedha inayotolewa na NMB ili kuongeza tija na ukuaji wa biashara zao.

Kwa upande wake, Kaimu Meneja wa NMB Kanda ya Kati, Amos Mubusi, alisema mikutano ya aina hiyo ni fursa ya kipekee kwa benki na wafanyabiashara kubadilishana mawazo, changamoto na suluhisho. Aliongeza kuwa hatua hiyo inaimarisha uhusiano wa kibiashara na kuchochea maendeleo ya uchumi wa taifa.

Baadhi ya wafanyabiashara walioshiriki walieleza kufurahishwa na mafunzo hayo, wakibainisha kuwa yamewasaidia kupata uelewa zaidi wa huduma za kifedha zenye manufaa kwa biashara zao, ikiwemo mikopo, bima, ulipaji kodi na suluhisho za kidijitali zinazorahisisha shughuli za kila siku.

Kupitia NMB Business Club, benki imekuwa ikiwafikia wafanyabiashara kote nchini kwa lengo la kuongeza maarifa ya kifedha na kuimarisha nafasi yao katika ukuaji wa uchumi wa Tanzania.












No comments:

Post a Comment