Dar es Salaam, 7 Julai 2025
Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania, Philip Besiimire (mwenye tisheti nyeupe), pamoja na Mkurugenzi wa Udhibiti wa Hatari na Utii wa Sheria, Agapinus Tax (wa kwanza kushoto), wametembelea banda la Vodacom katika viwanja vya Sabasaba na kupatiwa maelezo kuhusu televisheni janja (smart screen) inayotoa taarifa juu ya bidhaa na huduma mbalimbali za kampuni hiyo.
Tukio hilo limefanyika katika maadhimisho ya Siku ya Sabasaba, wakati wa Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam, yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere.
Vodacom inaendelea kutumia maonesho haya kama jukwaa la kuelimisha na kuhamasisha wateja kuhusu suluhisho za kidijitali na bidhaa bunifu zinazoboreshwa kila siku kwa mahitaji ya soko la kisasa.
No comments:
Post a Comment