Foreign Exchange Rates

CRDB Bank Advert_070325

Selcom Pesa Advert_110225

Selcom Pesa Advert_110225

Standard Chartered Advert_300125

Standard Chartered Advert_300125

Monday, 19 May 2025

SERIKALI YAJIPANGA KUIMARISHA UCHUMI KUPITIA UWEKEZAJI WA KIMKAKATI


Serikali imesema itaendelea kuchukua mwelekeo wa kimkakati wa kuwekeza katika maeneo yenye uwezo wa kukuza uchumi jumuishi na shindani na kwamba kipaumbele kimewekwa katika sekta ya usafiri kwa lengo la kurahisisha biashara, kuvutia uwekezaji wa ndani na wa kimataifa, na kuwaunganisha wazalishaji na masoko ya ndani na nje,ikiwa ni msingi wa kuharakisha maendeleo ya taifa kwa njia endelevu.


Akizungumza jijini Dar es salaam kwa niaba ya Waziri wa Viwanda na Biashara, Suleiman Jaffo, wakati wa maonesho ya kibiashara yaliyowakutanisha wawekezaji wenye nia ya kuja kuwekeza nchini na wafanyabiashara wa Tanzania yaliyoandaliwa na Benki ya Equity Tanzania ambapo zaidi ya washiriki 50 kutoka nchi 15 za afrika na nyingine za mabara ya ulaya wamehudhuria, Mkuu wa Chuo cha CBE,  Profesa Tandi Luoga ameeleza kuwa fursa za kipekee zilizopo katika sekta ya utalii hazipaswi kupuuzwa.


Profesa Luoga ameeleza kuwa ni muhimu kutumia vyema urithi wa asili na tamaduni zetu, Tanzania kwani inaweza kujipambanua duniani kama kivutio kikuu cha utalii na pia kama eneo lenye fursa nyingi za uwekezaji katika malazi, usafiri, na huduma za kijamii, na kuwa kujiunganisha na masoko ya kikanda kupitia EAC na AfCFTA kunatoa nafasi ya kukuza biashara na kuvutia mitaji mipya.


Kwa upande wake , Mkurugenzi Mtendaji wa Equity Bank Tanzania, Isabela Maganga ameeleza kuwa mkutano huu ni fursa ya kipekee ya kuunganisha wadau na kufungua milango ya uwekezaji unaoendana na vipaumbele vya taifa pamoja na malengo ya bara la Afrika kupitia AfCFTA, na kuwa zaidi ya wajumbe 236 kutoka Afrika, Ulaya, Asia na Mashariki ya Kati wamejiandikisha, jambo linaloonesha kuongezeka kwa hamasa ya kimataifa kwa mazingira ya biashara nchini.


Isabela pia ameelezea jinsi ambavyo Equity Group imekuwa ikiandaa misafara ya kibiashara katika masoko mbalimbali kama India, DRC, Kenya na China, na kufanikisha mikataba ya ubia, usambazaji bidhaa na ufadhili wa biashara, na kusisitiza kuwa benki yao iko tayari kuunga mkono safari ya uwekezaji Tanzania si kwa fedha tu, bali kwa kuunganisha, kuwezesha, na kuinua biashara zinazomilikiwa na wanawake na vijana.


Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania – TCCIA, Oscar Kisanga amesema tayari chemba hiyo kwa kushirikiana na serikali imeanza kuhamasisha wafanyabiashara watanzania kuchangamkia fursa ya soko huru la Afrika ili kujikwamua kiuchumi.


No comments:

Post a Comment