![]() |
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Bw Nickson Simon (alieshika mkasi) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kampeni ya ‘Wekeza NBC Shambani Ushinde’ inayoratibiwa na benki ya NBC mahususi kwa wakulima zao la ufuta mkoani Pwani wakati wa hafla ya uzinduzi iliyofanyika mapema jana wilayani Kibaha, mkoani Pwani. Wengine ni pamoja na Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo wadogo na wakulima kutoka Benki ya NBC, Bw Raymond Urassa (kulia), na wadau mbalimbali wa kilimo kutoka mkoa huo. |
Kibaha, Pwani - Mei 7, 2025: Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), imetambulisha kampeni yake ya ‘Wekeza NBC Shambani Ushinde’ kwa wakulima wa zao la ufuta mkoa wa Pwani ikiwa ni muendelezo wa jitihada za benki hiyo kuchochea kasi ya ukuaji wa sekta ya kilimo kupitia uchumi jumuishi unaochagizwa na huduma rasmi za kifedha.
“Hatua hii itasaidia kwa kiasi kikubwa kuhamasisha wakulima wetu kugeukia huduma rasmi za kifedha na hivyo kuchochea uchumi jumuishi. Hii ni hatua kubwa sana ikilinganishwa na tulipotoka miaka kadhaa iliyopita ambapo wakulima na wafugaji walikuwa hawaaminiki na taasisi za kifedha kutokana na kutokuwa waaminifu na wengine kutokuwa na dhamana.’’ Aliongeza.
Akifafanua zaidi kuhusu kampeni hiyo , Bw Urassa alisema walengwa wa kampeni hiyo ni wakulima wa zao la ufuta kupitia vyama vya msingi, vyama vikuu vya ushirika na mkulima mmoja mmoja ambao wanahudumiwa na benki hiyo.
“Lengo la kampeni hii ni kuwahamasisha wakulima wa zao la ufuta kwenye mkoa wa Pwani kutunza fedha zao kwenye mifumo rasmi ya kifedha hasa benki badala ya kutunza kwenye mifumo isiyo rasmi. Tunawakaribisha sana kufungua akaunti zao za NBC Shambani ili wawe kwenye nafasi ya kushinda zawadi hizi zikiwemo pikipiki na ‘laptop.’’ Alisema.
Akizungumza kwa niaba ya wakulima hao, Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Pwani (CORECU), Mussa Hemedi Mng'eresa aliwahimiza wakulima mkoani humo kutumia vema ujio wa kampeni hiyo kujinufaisha kupitia fursa mbalimbali zinazoambatana na kampeni hiyo ikiwemo zawadi, elimu ya fedha, mikopo na huduma nyingine ikiwemo bima za afya na mazao.
No comments:
Post a Comment