Euromoney:
- Benki Bora ya Uendelevu Tanzania
- Benki Bora ya Wateja Maalum Tanzania (kwa mwaka wa tatu mfululizo)
- Benki Salama Zaidi Nchini Tanzania
- Kinara wa Uwajibikaji kwa Jamii Tanzania 2025
- Afisa Mtendaji Mkuu Bora wa Benki Tanzania 2025 (Tuzo hii ilitolewa kwa CEO Ruth Zaipuna)
“Ni heshima kubwa kwetu kutambuliwa na Euromoney na Global Banking & Finance Magazine kwa uongozi wetu katika Ufadhili Endelevu na Huduma kwa Wateja Maalum,” alisema Bi. Zaipuna. “Tuzo hizi sita ni ushahidi wa juhudi na kujitolea kwa wafanyakazi wetu, imani kubwa ambayo wateja wetu wameendelea kutuonesha, na dhamira thabiti tuliyonayo ya kujenga mustakabali wa ustawi, ujumuishaji, na maendeleo endelevu kwa nchi yetu.”
"Sisi kama Benki ya NMB, uendelevu si tu ni wajibu wa kibiashara bali ni hitaji la kimkakati linalochangia uimara wa biashara, kuchochea ubunifu, kuongeza ushindani, na kuhakikisha upatikanaji wa thamani ya kudumu. Kwa kuufanya uendelevu kuwa kiini cha mkakati wetu wa biashara, tunawahakikishia wadau wetu thamani ya kudumu na kuwa na athari chanya kwa jamii tunazozihudumia."
Benki ya NMB pia imepata heshima ya kutambuliwa kama Benki Salama Zaidi nchini Tanzania kutokana na dhamira yake thabiti katika maendeleo ya kiteknolojia na rasilimali watu.
“Tuzo hii ni matokeo ya moja kwa moja ya uwekezaji wa kimkakati katika ubunifu na hatua madhubuti za usalama wa mtandao, hali inayowezesha uwepo wa mazingira ambayo yanafanya wateja zaidi ya milioni 8.6 kuwa na imani na uimara wa kifedha wa Benki ya NMB na usalama wa fedha zao.
"Tumejidhatiti kukuza uwezo wetu na kuhakikisha ufanisi wa kifedha wa kudumu, tutaendelea kuwekeza katika teknolojia na rasilimali watu ili kukidhi mahitaji anuwai ya wateja wetu tunaowathamini kwa moyo wote," alihitimisha Bi. Zaipuna.
Akizungumzia tuzo hizo, Mhariri Mkuu wa Euromoney, Bi. Louise Bowman, alisema, “Benki ya NMB imedhihirisha kuwa taasisi kinara wa maendeleo endelevu nchini Tanzania na barani Afrika kupitia mipango yake ya kimkakati inayozingatia uwiano wa uwajibikaji wa kimazingira, athari chanya kwa jamii, na ukuaji wa kifedha.”
Tuzo hizi zinabainisha dhamira ya Benki ya NMB katika uendelevu wa mazingira na jamii, sambamba na kutoa masuluhisho bora ya kifedha yenye viwango vya kimataifa, ambayo yanawawezesha wateja na kuchochea maendeleo jumuishi ya kiuchumi. Kutambuliwa huku ni uthibitisho wa maono ya kimkakati ya Benki ya NMB katika kuendeleza Ukuaji Jumuishi na Maendeleo Endelevu, huku ilipanua wigo wa upatikanaji wa huduma za kifedha kwa Watanzania wote.
Benki ya NMB inaendeleza kwa dhati dhamira yake ya kuzingatia viwango vya juu kabisa vya ubora wa huduma za kibenki, kuendeleza ubunifu, na kuchangia kikamilifu katika maendeleo endelevu ya Tanzania chini ya uongozi wa ushindi wa Bi. Zaipuna.
No comments:
Post a Comment