Dar es Salaam, Aprili 2025 – Stanbic Bank Tanzania imezindua rasmi huduma ya eMkopo, mkopo wa kidigitali uliobuniwa mahsusi kwa ajili ya watumishi wa umma, kupitia ushirikiano rasmi na Mfumo wa Serikali wa Watumishi Portal (https://ess.utumishi.go.tz).
Huduma hii inawawezesha watumishi wa umma nchini kuomba na kupata mkopo wa hadi TZS milioni 200, kwa kipindi cha kurejesha cha hadi miezi 108 (sawa na miaka 9), kwa njia rahisi na ya kidigitali bila kulazimika kutembelea matawi ya benki.
Akizungumza wakati wa uzinduzi, Emmanuel Mahondanga, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Stanbic Bank alisema:
"Uzinduzi wa eMkopo unaashiria hatua kubwa katika utoaji wa huduma za kifedha zinazozingatia mahitaji ya sasa. Kwa kuunganishwa na mfumo wa serikali wa Watumishi Portal, tunarahisisha mchakato mzima wa upatikanaji wa mikopo kwa watumishi wa umma – kwa njia ya haraka, salama na rafiki kwa mtumiaji. Hii ni sehemu ya dhamira yetu ya kuongeza ujumuishwaji wa kifedha na kuchochea ustawi wa wateja wetu."
Naye Priscus Kavishe, Meneja Mwandamizi wa Mauzo na Upatikanaji Wateja aliongeza:
"eMkopo ni matokeo ya ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi, unaolenga kuwahudumia kwa ufanisi watumishi wa umma. Kupitia Watumishi Portal – ambayo ni jukwaa rasmi la Serikali – mteja anaweza kuomba mkopo wa hadi TZS milioni 200 kwa njia ya kidigitali, na kuurejesha kidogokidogo kwa kipindi cha hadi miaka 9. Tunahakikisha huduma hii inawafikia kwa urahisi na kwa masharti rafiki."
Ili kuomba mkopo huu, mtumishi wa umma anapaswa kuingia kwenye Watumishi Portal kupitia kiungo: https://ess.utumishi.go.tz, kisha kuchagua Stanbic Bank kama benki anayopendelea kupata mkopo.
Kwa maelezo zaidi, tembelea tawi la Stanbic Bank lililo karibu nawe au wasiliana nasi kupitia namba ya bure: 0800 751 111.
Kwa mawasiliano zaidi:
Dickson Senzi
Meneja Mawasiliano
Stanbic Bank Tanzania
Simu: 0800 751 111
Barua pepe: Dickson.Senzi@stanbic.co.tz
Tovuti: www.stanbicbank.co.tz
Stanbic Bank Tanzania
Simu: 0800 751 111
Barua pepe: Dickson.Senzi@stanbic.co.tz
Tovuti: www.stanbicbank.co.tz
No comments:
Post a Comment