- TZS milioni 7.5 zimetolewa kama zawadi kwa wateja 15 waliotumia Visa Debit Card zao kwa miezi mitatu
- Washindi wengine watano wajishindia TZS 500,000 kila mmoja katika droo ya mwisho ya mwezi
- Mshindi wa gari jipya aina ya Suzuki Fronx kutangazwa siku chache zijazo
Katika droo ya mwisho ya mwezi iliyofanyika jijini Dar es Salaam, wateja watano—Coles Josette, Irene Charles Isaka, Chisora Kennedy, Abubakar Said Salim Bakhresa na Pietro Stella—wamejishindia TZS 500,000 kila mmoja. Washindi hao wanaungana na washindi wengine 10 kutoka droo za mwezi Februari na Machi, na kufanya jumla ya washindi kufikia 15 na jumla ya zawadi kufikia TZS milioni 7.5.
Wakati shauku ikiendelea kuongezeka, benki imethibitisha kuwa mshindi wa droo kuu ya kampeni hii—atakayeondoka na gari jipya aina ya Suzuki Fronx—atatangazwa rasmi katika siku chache zijazo. Hii itakuwa kilele cha kampeni ya Tap Kibingwa, ambayo imelenga kuwazawadia wateja waliotumia kadi zao kwaviwango vya juu na kwa uaminifu.
“Tap Kibingwa imekuwa njia ya kujenga imani katika huduma za kibenki za kidijitali,” alisema Irene Mutabihirwa, Meneja wa Kadi za Malipo – Benki ya Stanbic Tanzania. “Kupitia kampenihii, tumewazawadia wateja wetu kwa uaminifu wao na pia tumesaidia kuhamasisha tabia ya kufanya miamala salama, yaharaka na rahisi. Tumefunga hatua ya droo za kila mwezi nasasa tunajiandaa kumtangaza mshindi wetu mkuu.”
Kampeni ya Tap Kibingwa, iliyoanza mapema mwaka huu, iliwahamasisha wateja kuachana na malipo ya fedha taslimu na kuhamia kwenye malipo salama kwa kutumia kadi. Wateja waliotumia angalau TZS milioni 2 kwa mwezi walijumuishwa katika droo za pesa taslimu, huku waliotumia TZS milioni 5 au zaidi wakipata nafasi ya kushiriki katika droo zote mbili—ya kila mwezi na ile ya droo kuu.
Zaidi ya zawadi, kampeni hii imekuwa jukwaa la uelimishaji wa kifedha na ujumuishaji wa kidijitali, ikitoa hamasa ya kutumia mifumo ya kisasa ya kifedha na kuimarisha nafasi ya Benki ya Stanbic kama kinara wa ubunifu katika sekta ya kifedha nchini Tanzania.
“Kampeni hii imekuwa ni sherehe ya uaminifu kwa huduma za benki za kidijitali,” aliongeza Irene. “Tunajivunia kushirikiana na wateja wetu katika safari hii na tuna tazamia kuendeleza kasi hii kupitia bidhaa na huduma zinazo kidhi mahitaji yao ya kila siku.”
Kadri kampeni ya Tap Kibingwa inavyofikia tamati, Benki ya Stanbic inawashukuru wateja wote walioshiriki na inaahidi kuendelea kuboresha huduma za kidijitali zinazo waletea wateja thamani, usalama na urahisi katika miamala yao.
Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana na:
Jina: Dickson Senzi
Cheo: Meneja Mwandamizi; Mambo ya Nje, Mawasiliano, na Masuala ya Kampuni.
Barua pepe: Dickson.Senzi@stanbic.co.tz
Kuhusu Benki ya Stanbic, Tanzania
Benki ya Stanbic Tanzania ni mtoa huduma za kifedha anayeongoza nchini Tanzania, anayetoa bidhaa na huduma mbalimbali kwa wateja binafsi, biashara, na mashirika. Kama kampuni tanzu ya Standard Bank Group, Benki ya Stanbic, Tanzania inachanganya maarifa yake ya ndani na uwezo wa kimataifa wa Standard Bank kusaidia ukuaji na maendeleo ya wateja wake.
No comments:
Post a Comment