“Makubaliano yetu na wenzetu wa Hope Holding ni muendelezo wa jitihada za benki ya NBC tukilenga kutoa fursa kwa wateja wetu kufurahia miamala iliyorahisishwa wanapofanya manunuzi yao ya mavazi ya aina mbalimbali kwa ajili ya marafiki, familia, na wapendwa wao kuelekea kwenye sikukuu hizi za Eid el Fitr na Pasaka huku wakinufaika kupitia upendeleo wa bei kupitia punguzo la hadi asilimia 20 kwenye manunuzi kwenye maduka haya matano kwasasa yaliyopo hapa Morocco Square’’ alisema.
Kwa upande wake Bw. Decha pamoja na kuishukuru Benki ya NBC kwa makubaliano hayo alisema punguzo hilo la asilimia 20 ni msaada mkubwa kwa wateja wao wanaomiliki kadi za Benki ya NBC huku akionyesha kuvutiwa zaidi na jitihada za benki hiyo kuhamasisha matumizi ya kidigitali katika ufanyaji wa miamala kwa kuwa ni njia rahisi, salama zaidi kwa wateja na inawasaidia wao kama wafanyabiashara katika utunzaji wa kumbukumbu za malipo.
“Ushirikiano huu utakuwa na tija zaidi kuanzia kwa wateja wetu ambao kwasasa hawatalazimika kutembea na kiasi kikubwa cha fedha wanapokuja kufanya manunuzi na zaidi kwasasa wataweza kupata bidhaa zetu kwa punguzo la asilimia 20. Tunawakaribisha sana hususani kipindi hiki cha kuelekea Sikukuu za Eid el Fitr na Pasaka.’’ Alisema.
No comments:
Post a Comment