Kitomari Banking & Finance Blog is a premier site for banking, finance, business, economic, investment and stock market news as well as selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the World. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.
Foreign Exchange Rates
CRDB Bank Advert_070325
Selcom Pesa Advert_110225
Standard Chartered Advert_300125
DStv Advert_090724
Thursday, 21 November 2024
VODACOM TANZANIA YATOA ELIMU KUHUSU UTAPELI MTANDAONI
Dar es Salaam, 20 Novemba 2024: Kampuni ya Vodacom Tanzania Plc imetembelea soko la Makumbusho jijini Dar es Salaam kutoa elimu na kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu utapeli wa kimtandao. Zoezi limefanywa kwa lengo la kuwasaidia watumiaji wa mtandao namna ya kutambua na kuepuka matapeli katika mitandao ya simu.
“Tatizo la utapeli wa mtandaoni limekuwa likiongezeka kila siku ambapo watu wengi wamekuwa wahanga kwa kupoteza fedha zao bila kujua nini cha kufanya. Hivyo Vodacom tumekuja leo kutoa elimu na kuongeza uelewa kwa wananchi ili wajue jinsi ya kukubaliana na matapeli,” anasema Agapinus Tax, Mkurugenzi wa Udhibiti wa Hatari na Utii wa Sheria kutoka Vodacom Tanzania.
Agapinus anasema hili zoezi ni endelevu na litakuwa pia katika mikoa ya Rukwa na Morogoro ambayo, kwa mjibu wa takwimu, ni kati ya mikoa inayoongoza kwa vitendo vya utapeli wa mtandaoni.
No comments:
Post a Comment