Kitomari Banking & Finance Blog is a premier site for banking, finance, business, economic, investment and stock market news as well as selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the World. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.
Foreign Exchange Rates
CRDB Bank Advert_070325
Selcom Pesa Advert_110225
Standard Chartered Advert_300125
Tuesday, 19 November 2024
KAMATI YA BUNGE YA UWEZESHAJI YARIDHISHWA NA UTENDAJI KAZI WA TCB
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwezeshaji Taasisi za Umma imeridhishwa na utendaji kazi wa Benki ya Biashara Tanzania - TCB, huku ikiielekeza benki hiyo kuendelea kutoa gawio kwa serikali kuu ili fedha hizo zitekeleze miradi mingine ya kimkakati.
Kauli hiyo imetolewa Jijini Dar es salaam hivi karibuni na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Augustino Vuma wakati Kamati hiyo ilipotembelea benki hiyo ili kufahamu mikakati, utendaji kazi pamoja na mwelekeo wake kwa mwaka 2025.
Amesema pamoja na mambo mengine ushirikiano wa benki hiyo na taasisi nyingine za serikali ikiwemo Shirika la Reli Tanzania - TRC, katika utoaji wa huduma imetajwa kuwa kichocheo muhimu cha ukuaji wa uchumi nchini.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa - TCB, Adam Mihayo amesema benki hiyo itaendelea kushirikiana na serikali katika nyanja zote ikiwa ni pamoja na Kijamii na kiuchumi.
Itakumbukwa kuwa Kamati hiyo imekua ikifanya ziara yake ya kutembelea taasisi mbalimbali za Serikali ili kusikiliza changamoto zao, kuona utendaji wao wa kazi na kuwasilisha ripoti kwa serikali kuu.
No comments:
Post a Comment