CEO wa Tausi Africa Technologies Limited, Derick Kazimoto akiongea wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa Manka unaotumia Akili Memba (AI) wa kuchakata taarifa za mikopo. |
Dar es Salaam, Oktoba 24, 2024: Tausi Africa imezindua rasmi Manka, mfumo wa uchambuzi wa kifedha unaotumia teknolojia ya Akili Mnemba, uliobuniwa kuboresha tathmini za mikopo katika uchumi usio rasmi wa Tanzania. Mfumo huu unafanyia uchambuzi taarifa za benki na pesa za simu, likiwawezesha watoa huduma za kifedha kufanya maamuzi ya haraka na sahihi zaidi kuhusu mikopo. Kwa kupunguza muda wa tathmini za mikopo kutoka takriban saa 3 kwa mteja hadi chini ya dakika 2, Manka inalenga kuongeza ufanisi katika sekta ya kifedha na kusaidia ujumuishaji wa kifedha.
CEO wa Creditinfo Tanzania, Edwin Urasa akiongea wakati wakitangaza ushirikiano wao na Tausi Afrika katika ufanyaji kazi wa mfumo wa Manka. |
Uzinduzi huu ulifanyika Oktoba 24, 2024, katika hoteli ya Hyatt, Dar es Salaam, ukiwaleta pamoja wadau kutoka sekta ya benki na fedha ili kujadili athari zinazoweza kutokana na mfumo huu kwenye mazoea ya utoaji mikopo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi, Derick Kazimoto, Mkurugenzi Mtendaji wa Tausi Africa Technologies Limited, alisema, "Manka imeundwa ili kuboresha upatikanaji wa mikopo kwa kuwawezesha watoa huduma za kifedha kuwahudumia wateja wao kwa ufanisi zaidi. Kwa kuboresha tathmini za mikopo na kutoa maarifa kuhusu tabia za wateja, Manka inaziwezesha taasisi kutoa suluhisho za kifedha haraka zaidi na kwa njia ya kibinafsi, siyo tu katika mikopo, bali pia kwenye bidhaa mbalimbali za kifedha. Zaidi ya hayo, Manka inasaidia kuwalinganisha wateja na chaguo za kifedha zinazokidhi mahitaji yao vyema zaidi, hivyo kuongeza upatikanaji wa suluhisho bora za kifedha kwenye soko. Kipaumbele chetu ni kuwawezesha watoa huduma za kifedha kukidhi mahitaji ya wateja wao, hivyo kufungua fursa kwa ujumuishaji bora wa kifedha."
Mfumo huu unatumia Akili Mnemba kutoa uchambuzi wa kina wa hatari za mikopo na kuwatathmini awali watumiaji kutoka taasisi mbalimbali za kifedha kwa usahihi wa hali ya juu. Manka inaakisi dhamira ya Tausi ya "Kufungua upatikanaji wa fedha kwa uchumi usio rasmi wa Afrika" kwa kuchochea ujumuishaji wa kifedha na kuongeza upatikanaji wa mikopo kwa biashara ndogo na za kati (SMEs).
Manka inawakilisha uwajibikaji na hekima ya kifedha, sifa zilizochochewa na jina lake kutoka kabila la Wachagga. Thamani hizi zinaakisiwa ndani ya Manka, ikitoa uchambuzi wa kifedha ulio wazi na wenye maarifa, unaowezesha maamuzi ya busara na kuweka njia ya fursa zaidi za kifedha nchini Tanzania.
Ufanisi ambao Manka inaleta kwenye tathmini za mikopo utasaidia taasisi za kifedha kuwahudumia wateja vyema zaidi huku ikipunguza hatari zinazohusiana na utoaji wa mikopo, hasa katika sekta ambazo kwa jadi hazikuhudumiwa vya kutosha.
No comments:
Post a Comment