Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday, 27 August 2024

VODACOM, HUAWEI WAZINDUA MPANGO WA UJUZI WA KIDIGITALI KWA WOTE


DigiTruck, darasa la kidijitali linalotembea, ushirikiano kati ya Huawei na Vodacom Tanzania, litazinduliwa nchini Tanzania mnamo August 2024 kabla ya Vodacom Twende Butiama Cycling Tour 2024. Mpango huu unalenga kuwapatia Watanzania ujuzi wa msingi wa kidijitali na kuwaboreshea ujuzi na maarifa, ukilenga wanafunzi zaidi ya 5,500, wanawake, na vijana katika mikoa 10.


Darasa hili la kidijitali linalotembea linaonesha kujitolea kwao kuwawezesha Watanzania kupata ujuzi muhimu wa kidijitali, hususani kwa maeneo na watu walio na upungufu wa fursa. Kupitia programu maalum kwa shule za sekondari, vijana waliojiajiri, na wanawake wajasiriamali, DigiTruck inalenga kuwawezesha Watanzania na nyenzo wanazohitaji ili kufanikiwa katika ulimwengu unaozidi kuwa wa kidijitali.




No comments:

Post a Comment