Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Friday 30 August 2024

CRDB, VISA KUTOA PUNGUZO LA ASILIMIA 22 KWA ABIRIA WA QATAR AIRWAYS


Dar es Salaam, Tarehe 26 Agosti 2024: Benki ya CRDB kwa kushirikiana na wabia wake wa kimkakati ambao ni kampuni ya Visa International imetangaza kutoa nafuu ya nauli ya asilimia 22 kwa abiria wa Shirika la Ndege la Qatar wanaolipia tiketi zao kwa kutumia kadi za Tembocar Visa. 

Nafuu hiyo inajumuisha punguzo la asilimia 12 litakalotolewa na kampuni ya Visa International pamoja na asilimia 10 ya fedha taslimu itakayorudishwa kwenye akaunti ya mteja wa Benki ya CRDB baada ya kulipia tiketi yake.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa wakati wa kuzindua kampeni hiyo itakayodumu kwa miezi sita, Kaimu Mkurugenzi wa Wateja wa Awali na Kati wa Benki ya CRDB, Muhumuliza Buberwa amesema ushirikiano huu unalenga kujunga utamaduni kwa wateja kutumia kadi kufanya malipo na kuachana na matumizi ya fedha taslimu. 

“Punguzo hili la asilimia 22 ni sehemu ya motisha kwa wateja kujenga utamaduni wa kutumia kadi kufanya malipo. Nitumie nafasi hii kuwakaribisha wateja wetu wanaotaka kusafiri kutumia ndege za Shirika la Ndege la Qatar ili kunufaika na punguzo hili ili. ,” amesema Paul huku akibainisha kuwa punguzo hilo pia linatosha kwa abiria kununua zawadi kwa ajili ya wapendwa wao pindi wawapo safarini.


Kaimu Mkurugenzi huyo amesema ushirikiano wa Benki ya CRDB, Visa International na Shirika la Ndege la Qatar unazijumuisha taasisi mbili kubwa zenye ubora unaotambulika ndani na kimataifa uliozifanya zitunukiwe tuzo za aina tofauti.

Tangu mwanzoni mwa miaka ya 2000, Paul amesema Benki ya CRDB imetunukiwa takriban tuzo 200 a ndani na kimataifa ikiwamo tuzo za utoaji wa huduma bora za Visa, wakati Shirika la Ndege la Qatar likishinda tuzo ya shirika bora la ndege zinatolewa na kampuni ya Skytrax mara nane kati ya mwaka 2011 mpaka mwaka 2024.

Shirika hilo pia limeshinda tuzo ya shirika lenye daraja bora la biashara duniani (world’s best bisness class), ukumbi bora wa daraja la biashara duniani (world’s best business class lounge) na shirika bora la ndege ukanda wa Mashariki ya Kati.

“Benki ya CRDB na Shirika la Ndege la Qatar pia tunafanana kwenye ubunifu. Benki yetu ndio kiongozi katika ubunifu wa huduma na bidhaa zinazokidhi mahitaji na matarajio ya wateja wetu vivyo hivyo kwa Shirika la Ndege la Qatar ambalo limeshinda tuzo za kimataifa kutokana na ubunifu wake. Vilevile, sisi sote wawili tunajali na kuyatunza mazingira,” ameeleza Buberwa.


Meneja Mkazi Shirika la Ndege la Qatar, Isaack Wambua amesema ndege zao zenye makao makuu katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hamad uliopo jijini Doha ambao umeshishinda tuzo ya uwanja bora wa ndege duniani mara tatu kuanzia mwaka 2021, zinatua katika viwanja vingine 170 duniani kote hivyo kuwapa abiria wao uhakika wa kufika popote wapatakapo huku Benki ya CRDB ikiwahakikishia kukamilisha safari zao kwa gharama nafuu. 



“Punguzo hili la Benki ya CRDB litakalodumu mpaka Desemba mwaka huu, linawahusu wateja wetu wote wanaotumia kadi za Tembocard Visa ambao ni zaidi ya milioni nne.

Kwa kuwa tunatambua kwamba wanazo biashara nje ya nchi na huwa wanasafiri kwa malengo tofauti, tunaamini wataitumia fursa hii kusafiri na ndege za Shirika la Qatar kwenda wanapopataka,” amesema Wambua.







No comments:

Post a Comment