Ndunguru ametoa wito huo alipofungua semina ya wajasiriamali wanawake na vijana iliyoandaliwa na Taasisi ya CRDB Bank Foundation na kufanyika makao makuu ya Benki ya CRDB.
“Ili kuwawezesha zaidi wajasiriamali wanawake na vijana, ni muhimu wadau wote wa maendeleo wakashiriki. Serikali pekee haitoweza kutatua changamoto zote zinazotukabili kwa kasi tunayoitarajia. Lazima tufanye kazi pamoja ili kujenga mazingira ambayo kila mwanamke na kijana anapata fursa ya kufanikiwa.
Niipongeze CRDB Bank Foundation kwa kuja na programu hii ambayo inalenga kuboresha biashara za vijana na wanawake kwa kuwapa mafunzo na ushauri wa namna bora ya kusimamia na kuendesha biashara zao, kuwapa mitaji wezeshi, na kuwaunganisha na masoko ya ndani na nje ya nchi,” amesema Ndunguru.
Katibu mkuu huyo pia ameusifu utaratibu wa CRDB Bank Foundation kushirikiana na vikundi na taasisi za uwezeshaji wa wanawake na vijana nchini katika sekta mbalimbali za maendeleo kwamba unawafanya wananchi wajione ni sehemu ya benki na wanawajibika kwa maendeleo yao binafsi baada ya kupewa kemkem zilizopo kuweza kujikwamua kiuchumi.

Katibu mkuu ametoa pongezi hizo baada ya Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Foundation, Tully Mwambapa kueleza kuwa malengo ya taasisi hiyo ni kutoa elimu ya fedha, kukuza ubunifu na teknolojia, kuwawezesha wajasiriamali kwa mtaji, kuongeza ujumuishi wa kifedha na kiuchumi ili kuboresha maisha ya vijana na wanawake.
Ili kuwafikia wanufaika wengi zaidi, Tully amesema wanashirikiana na wadau wa ndani na wa kimataifa BUTA VICOBA Endelevu, Bunju Women Entrepreneurs (BWE), Mbweni Women Empowerment (MWE), Eden Group, UWABISORA, Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) na Tume ya TEHAMA (ICTC), Sokoine University Graduate Entrepreneurs Cooperative (SUGECO), pamoja na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
“Wanawake na vijana ni makundi yanayokabiliwa na changamoto nyingi za kiuchumi ndio maana Benki yetu ya CRDB kupitia CRDB Bank Foundation iliona kuna kila sababu ya kutoa elimu na kuwapa mitaji wezeshi wale wanaokidhi vigezo ili kujenga uchumi jumuishi na shirikishi ili kuwa na maendeleo endelevu,” amesema Nsekela.
No comments:
Post a Comment