Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday 9 July 2024

DStv YAJA NA "MBUNGI BAMPA 2 BAMPA"

  • Ni kuelekea msimu wa Soka kimataifa
  • Wateja wa DStv kushuhudia ligi kubwa duniani live
  • Wateja wa vifurushi vya chini nao wamo!
Ule mchakamchaka wa ligi maarufu duniani umewadia tena ambapo wakongwe wa Burudani - DStv kama ada wametangaza rasmi kuwa wataonyesha mubashara mitanange ya ligi za Ulaya zikiwemo Premier League, Serie A, La Liga na bila kusahau michuano kabambe ya UEFA Champions League.

Msimu huu DStv wanasema ni Mbungi Bampa2Bampa ikimaanisha kuwa wateja wa DStv wajiandae kupata uhondo wa michuano hiyo mubashara kwenye televisheni zao au vifaa vingine kupitia chaneli za SuperSport.

Akitangaza habari hizo njema kwa wapenzi wa soka hapa Tanzania, Mkuu wa Masoko wa MultiChoice Tanzania, Ronald Shelukindo amesema msimu huu itakuwa ni burudani ya aina yake kwa wateja wote wa DStv kwani hawatapitwa na uhondo huo ikiwa wamelipia vifurushi vyao.

Shelukindo amesema kwa wale wateja wa kifurushi cha DStv Bomba cha shilingi 24,000 watashuhudia mechi 2 za EPL, 2 za La Liga na 2 za Serie A kila wiki, huku wateja wa kifurushi cha DStv Shangwe watashuhudia mechi zote za La Liga na Serie A, huku wakishuhudia meci 2 EPL na baadhi ya mechi za UCL.

Uhondo wa kufa mtu unapatikana katika kifurushi cha DStv Compactna kuendelea ambapo mteja atashuhudia mecho zote za EPL, Serie A, La Liga huku wale wateja wa DStv Compact Plus wao mbali na mech izote hizo, watashuhudia michuano ya UEFA Champions League.

Mbungi la msimu huu si la kitoto kwani Manchester City, chini ya mwamba Pep Guardiola, hawatataka kupoteza ufalme wao hivyo watapigana kufa na kupona kuutetea ubingwa wao huku manusura wa ubingwa huo Arsenal wakiwa na kiu ya kuutwaa baada ya kulikosakosa kombe hilo msimu uliopita.

Wababe ewngine wa soka la Uingereza Chelsea, Manchester United na Liverpool nao watataka kurekebisha makosa yao na kufanya maajabu msimu huu kitu ambachi kinaifanya EPL kuwa ligi ya moto sana.

Wahenga walisema kwenye msafara wa Mamba, na Kenge nao wamo! Je msimu huu Kenge kama Newcastle United, Aston Villa, Tottenham Hotspur na wengineo watataka kuwa Mamba halisi? Kazi yetu ni moja tu, kukodolea macho SuperSport Ndani ya DStv pekee!

Huko Uhispania nako litakufa jitu wakati miamba ya La Liga Real Madrid hawatakubali kiwingu hasa ukizingatia kuwa wamemsajili Kylian Mbappe na hivyo kuimarisha zaidi kikosi chao cha mauaji kinachoongozwa na mtaalamu Carlo Ancelotti.

Huku nako moto utawaka, kwani wababe wengine nao wanalitaka kombe hilo kwa udi na uvumba. Wabishi kama Internazionale, chini ya Simone Inzaghi AC Milan, Juventus, Atalanata na Napoli ambao wana meneja mpya Antonio Conte kila mmoja atakuwa na kiu ya ubingwa kitendo kinachoifanya La Liga kuwa moto wa kuotea mbali.

Kupitia SuperSport Ndani ya DStv pekee, huna sababu ya kubanduka kwani ni mbungi bampa2bampa – huku EPL, Serie A, La Liga… kule FA Cup na michuano ya UEFA (Champions League, Europa League na Conference League). Hakik ani Mbungi Bampa2Bampa!

Cha kufurahisha zaidi ni kwamba unaweza kushuhudia michuano yote hii popote ulipo kwa kutumia App MyDStv kwenye simu au kompyuta yako. Hakikisha unalipia kiurushi chako usipitwe na uhondo huu. Kulipia kwa urahisi kwa kutumia simu yako bofya *150*53#

Kwa wale ambao bado hawajajiunga na DStv, sasa kuna ofa kabambe ambapo seti ya DStv ni shilingi 49,000 tu! Hii ni seti kamili ikiwa na Dish, dikoda na vifaa vyote vya kufungia DStv. Unakosaje uhondo huu kwa bei mchekea? Nunua set yako ya DStv leo na wewe uwe mtu kati ya watu!

No comments:

Post a Comment