Waziri Mkuu Majaliwa alitoa pongezi hizo alipotembelea banda la maonyesho ya huduma za benki hiyo mahususi kwa wadau wa sekta ya afya lililopo kwenye kongamano la Afya Kitaifa lililoandaliwa na Taasisi ya Benjamin Mkapa (BMF) katika ukumbi wa JNICC Dar es salaam.
Akizungumza mara baada ya kupokea taarifa fupi kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Mahusino ya Umma wa benki ya NBC Bw. Godwin Semunyu kuhusu jitihada mbalimbali zinazofanywa na benki hiyo kwenye sekta afya, Waziri Mkuu Majaliwa alisema serikali inathamini mchango mkubwa unaofanywa na benki hiyo pamoja na wadau wengine katika kusaidia sekta hiyo muhimu.
“Ni juzi tu nimetoka kuongoza mbio za NBC Dodoma Marathon zilizofanyika huko Dodoma ambapo jumla ya milioni 300 zilikusanywa na benki ya NBC kwa ajili ya kusaidia jitihada mbalimbali za kiafya hususani kuokoa Maisha ya mama na mtoto. Huko Zanzibar pia wamekuwa wakifadhili huduma za uchunguzi wa bure kwa wanawake wajawazito kupitia huduma ya kliniki inayotembea pamoja na jitihada nyingine nyingi…hongereni sana NBC,’’ alipongeza.
Akiwa kwenye banda hilo pia Waziri wa Afya , Ummy Mwalimu aliipongeza benki hiyo kwa jitihada hizo kwenye sekta ya afya huku akiahidi kuendelea kushirikiana na benki hiyo katika kutekeleza miradi mbalimbali kwenye sekta ya afya hususani ile inayolenga afya ya mama na mtoto.