Meneja Mkuu wa Puma Energy Tanzania, Fatma Abdallah akiongea na wateja, washirika na wadau wao mbalimbali wakati walipoandaa futari ya pamoja mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. |
Akisisitiza katika malengo ambayo huwakutanisha kwa pamoja Waislamu wote nchini wakati wa mfungo wa Ramadhan, kwa niaba ya Sheikh Mkuu wa Dar es Salaam, Sheikh Walid Alhad Omar, Sheikh wa Wilaya ya Temeke, Zaira Mkologoye ambaye alikuwa ni mgeni rasmi, amebainisha kuwa mwezi mtukufu ni fursa ya kuimarisha upendo na mshikamano sio tu kwa waumini pekee bali na jamii nzima kwa ujumla.
“Kwa ajili ya mwezi huu mtukufu, ninawaomba tujitahidi kuyafuata mafundisho ya Uislamu kwa kuonyesha upendo na matendo ya huruma. Tuwasaidie wale wenye uhitaji, na kudumisha umoja miongoni mwa jamii yetu. Kwa kufanya matendo memo na ya ukarimu, sio tu kwamba tunatimiza wajibu wetu wa kiimanini bali pia tunachangia jamii yenye mshikamano na kujali zaidi. Ningependa kuwapongeza Puma Energy Tanzania kwa shughuli zao za kijamii, na ninawaasa muendelee na miradi hii ili kuzinufaisha jamii zenye uhitaji zaidi,” alimalizia Sheikh Walid Alhad Omar.
Akishukuru, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Dk. Selemani Majige ametoa shukrani zake za dhati kwa mgeni rasmi Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam kwa kuungana na kampuni ya Puma Energy Tanzania na wadau wake kushiriki shughuli hii muhimu ya Iftar, akasisitiza kuendeleza ushirikiano wa kibiashara unao ifanya kampuni ya Puma Energy Tanzania iendelee kufanya vizuri sokoni huku aki ahidi jitihada zaidi katika kuboresha huduma zetu ili kutoa huduma bora zaidi kwa wateja wetu na gawio stahiki kwa wanahisa. Mwenyekiti alimalizia kwa kuwatakia wakristo wote heri ya sikuu ya pasaka.
Tukio hili lilihudhuriwa na washirika, wadau, na wafanyakazi wa kampuni hiyo ya usambazaji wa mafuta na nishati nchini. Pia, ilitoa fursa ya kipekee ya kukutana na kubadilishana mawazo juu ya namna bora ya kuhudumia jamii ya Watanzania.
Miongoni mwa jitihada za Puma Energy Tanzania ni kupitia mradi wa kuwezesha shule za msingi za umma ambao unaunga mkono programu ya WASH inayolenga kuboresha mahudhurio ya wanafunzi, kuendelea na masomo, na kuwa na matokeo bora ya elimu. Pia imekuwa na mkakati endelevu wa kutoa elimu ya usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi nchi nzima.
KUHUSU KAMPUNI YA PUMA ENERGY TANZANIA
Puma Energy Tanzania ni kampuni ya mafuta iliyosajiliwa ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kampuni inamilikiwa kwa pamoja na serikali ya Jamhuri ya Muungano (Kupitia Msajili wa Hazina) pamoja na Puma Energy Group kupitia kampuni yao tanzu ya Puma Investments Limited, kila moja ikiwa na umiliki wa hisa asilimia 50 kwa asilimia 50. Kampuni ya Puma Energy ni ya mkondo wa kati kimataifa katika masula ya usambazaji mafuta kupitia mtandao wa vituo vyake takribani 80 nchi nzima, wateja wakubwa na wakatai zaidi ya 200, nishati safi ambayo inasaidia mapambano dhidi ya kupunguza utoaji wa hewa ya ukaa, vilainishi vya vyombo vya moto na mitambo, na pia ni kampuni inayojihusisha na uhifadhi mkubwa wa mafuta.
No comments:
Post a Comment