Toleo hili jipya la 'Smart Kitochi+' ni sehemu ya juhudi za Vodacom kuwapeleka wateja wake kwenye matumizi ya kidigitali, ikiwa ni pamoja na mtandao wa 4G, ambao bado una watumiaji wachache ikilinganishwa na idadi ya watumiaji wa simu za mkononi nchini Tanzania.
"Tunajivunia kuwa mtandao unaoongoza nchini, tukitoa huduma za kidigitali za ubunifu kwa zaidi ya wateja milioni 21. Kuwa na idadi kubwa ya wateja pekee haitoshi; tunataka wateja wetu wanufaike na mapinduzi ya kidigitali yanayoendelea na ubunifu mkubwa tunaoingiza kwenye bidhaa zetu. Kwa kuanzisha bidhaa za kisasa kama 'Smart Kitochi+' tunaamini tutachochea wateja wengi zaidi kuhama kutoka kwenye mfumo wa 2G na kuanza kufurahia huduma mbalimbali za kidigitali zinazotolewa na mtandao wetu wa kasi wa 4G na 5G uliosambaa nchini na hatimaye kuongeza matumizi ya simujanja ambayo kwa sasa ni asilimia 32," alifafanua Bi. Linda.
Akizungumzia simu hiyo mpya, Mwenyekiti wa Chama cha Viziwi Tanzania (TLB) Bw. Luis Benedicto aliisifia simu hiyo akikiri kuwa itakuwa mkombozi kwa watu wenye ulemavu wa kusikia na kuona.
"Tulikuwa tumetengwa na kubanwa katika matumizi ya simu za mkononi, kwani nyingi hazikuwa rafiki kwa watu wenye ulemavu wa kusikia na kuona. Kuzinduliwa kwa simu hii kutatusaidia sio tu kufurahia huduma za mawasiliano kutoka Vodacom bali pia kuimarisha mwingiliano wetu na wengine na kutumia simu hizi kwa manufaa ya kijamii na kiuchumi," alielezea Bw. Benedicto.
Uzinduzi huu unakuja baada ya hivi karibuni kampuni hiyo kuanzisha dawati maalum kwa ajili ya kuhudumia wateja wasioona baada ya kuanzisha dawati kama hilo kwa ajili ya wateja wenye ulemavu wa kusikia mwaka jana.
Juhudi za kampuni hiyo katika kuzingatia na kuboresha maisha ya wateja wake ili kupunguza au kufuta kabisa utofauti uliopo wa kidigitali kwa watu wenye ulemavu zimeifanya iwe miongoni mwa watia saini wa miongozo ya GSMA kwa kuchochea ushirikishwaji wa kidigitali kwa watu wenye ulemavu. Miongozo hiyo huweka misingi ya hatua za kuchukua pamoja na kinachotakiwa kufanywa na mtoa huduma za simu za mkononi ili kupunguza pengo katika upatikanaji wa huduma pamoja na matumizi ya huduma hizo.
No comments:
Post a Comment