Foreign Exchange Rates

Standard Chartered Advert_300125

Standard Chartered Advert_300125

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

Thursday, 4 April 2024

BOA BANK YAFUTURISHA WATEJA NA KUAHIDI KUIMARISHA ZAIDI HUDUMA

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bank of Africa, Wasia Mushi (wa pili kulia) akiwa na wateja na wageni walioalikwa.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bank of Africa, Wasia Mushi akiongea na wateja walioalikwa kwenye Iftar iliyoandaliwa na Benki hiyo jijini Dar es Salaam.
Sheikh Ramadhan Shareef Koba kutoka BAKWATA akitoa mawaida katika Iftar iliyoandaliwa na Bank of Africa.
Wateja na wageni walioalikwa wakiwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Wasia Mushi.
Ibada kwa njia ya Kaswida pia ilikuwepo.

Bank of Africa Tanzania (BOA) ipo mbioni kuandaa Jukwaa la kuwakutanisha pamoja wafanyabiashara wa ndani ili kutoa fursa ya kuonyesha bidhaa na huduma zake katika juhudi za kukuza ushirikiano baina yake na wateja sambamba na kuchochea biashara na uchumi wa nchini kwa maendeleo ya taifa zima.


Akizungumza katika futari iliyoandaliwa kwa wateja wake mkoani Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Wasia Mushi, alisema kwamba lengo la kuandaa Jukwaa hilo la kibiashara ni kuwaleta pamoja wafanyabiashara ili waweze kubadilishana uzoefu.


“Lengo kuu la Jukwaa hilo ni wafanyabiashara kuongeza na kupanua wigo wa biashara zao na kuzileta pamoja na kuzionyesha na kufungua fursa ya biashara na kupanua wigo wa mahusiano na mitandao ya kibiashara,” alisema Bw. Mushi

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Wasia Mushi (kulia) akikaribisha wateja wa Bank of Africa katika Iftar.

Alisema pia benki hiyo itaendelea kuandaa makongamano na mafunzo kwa wajasiriamali na wafanyabiashara kuhusu mambo ya kodi, usimamizi wa fedha na huduma zingine za kibenki kuendelea kusogezwa karibu na wateja katika juhudi za kuwarahisisha wateja wao huduma za kibenki.

Kaimu Mkurugenzi wa Bank of Africa akiwashukuru wafanyakazi wenzake kwa kufanikisha maandalizi ya Iftar kwa ajili ya wateja.

Bw. Mushi aliongeza pia benki hiyo itaboresha na kuendelea kukuza huduma zake za kibenki ikiwamo huduma za uwakala, simu na mifumo yote ya matumizi ya teknolojia (Tehama) katika jitihada za kukuza biashara na kuchochea ukuaji wa uchumi wa nchini.

“Benki yetu inatoa ahadi kuendelea kutoa huduma bora na uwajibikaji wa hali juu katika kuhakikisha ustawi wa wateja wetu na kuchochea maendeleo uchumi katika sekta mbalimbali hapa nchini,” aliongeza Bw. Mushi.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji huyo alisema kuwa ni heshima kwa uongozi wa Benki kuandaa Iftar kwa wateja wa benki hiyo, pamoja na kukuza hisia za jumuiya kati ya imani mbalimbali.

Alisisitiza zaidi umuhimu wa kushiriki pamoja kupata Iftar katika mwezi mtukufu wa Ramadhani na umuhimu wa kuishi pamoja kidini na kuheshimiana kwa ajili ya kudumisha amani, maelewano na ustawi wa jamii.

Aliwathibitishia wateja wa benki hiyo kuhusu mkakati makini wa benki kuboresha huduma zake za kifedha kuendana na matakwa yao ikilenga zaidi kukuza makundi ya Biashara Ndogo na za Kati (SME) ambazo ni sehemu muhimu katika kuchangia ukuaji wa Pato la Taifa.

Pia alieleza ni kwa jinsi gani Benki imejipanga kuboresha huduma zake katika kuhudumia makundi yote ya wateja kuanzia wateja binafsi, wafanyabiashara na makampuni katika kufanikisha ajenda za Serikali za kukuza ushirikishwaji wa kifedha nchini.

Kwa upande wake Sheikh Ramadhan Shareef Koba, kutoka Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA) aliipongeza Bank of Africa Tanzania, kwa kuandaa Iftar, huku akigusia moja ya hadithi za Mtume Muhammad, kwamba “anayemlisha muumini aliyefunga hulipwa sawa na baraka zote za waliokaribishwa.”

No comments:

Post a Comment