Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Thursday 28 March 2024

DKT. NCHEMBA AKUTANA NA MKURUGENZI MPYA WA TBL

Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Kampuni ya Tanzania Breweries Plc, Bi. Michelle Kilpin, akizungumza kuhusu mchango wa Kampuni yake katika maendeleo ya uchumi, alipofika kujitambulisha kwa Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), ofisini kwake (Treasury Square), jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akipeana mkono na Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Kampuni ya Tanzania Breweries Plc, Bi. Michelle Kilpin, baada ya kufika Ofisi za Hazina (Treasury Square), jijini Dodoma, kujitambulisha, ambapo Mkurugenzi Mtendaji huyo ameipongeza Serikali kwa kuboresha mazingira ya kufanya biashara na kuahidi kuwa Kampuni yake itaendelea kuchangia maendeleo ya nchi kupitia program mbalimbali za kusaidia jamii na kulipa kodi.
Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Kampuni ya Tanzania Breweries Plc, Bi. Michelle Kilpin, akisaini kitabu cha wageni, alipofika kujitambulisha kwa Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), ofisini kwake (Treasury Square), jijini Dodoma, ambapo ameahidi kuendelea kuchangia katika shughuli za kijamii katika kusukuma kurudumu la maendeleo.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akisikiliza maelezo ya Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Kampuni ya Tanzania Breweries Plc, Bi. Michelle Kilpin (kulia), kuhusu Kampuni yake kuendelea kuchangia maendeleo ya jamii.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Kampuni ya Tanzania Breweries Plc, Michelle Kilpin (wa tatu kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe kutoka Wizara ya Fedha na TBL baada ya kumalizika mkutano kati yao, katika Ukumbi wa Waziri wa Fedha (Treasury Square), jijini Dodoma.

No comments:

Post a Comment