Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Wednesday, 27 March 2024

AKIBA COMMERCIAL BANK YAANDAA FUTARI KWA WATEJA NA WADAU WAKE


Akiba Commercial Bank (ACB) imeandaa hafla ya Futari kwa kuwaalika Wateja, Wafanyakazi pamoja na Wadau mbalimbali wa benki hiyo.

Katika hafla hiyo iliyofanyika tarehe 25 Machi, 2024 katika Hoteli ya Serena Mkurugenzi Mtendaji wa ACB, Bw. Silvest Arumasi alitumia fursa hiyo kuwapongeza Waislamu wote kwa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan, na amewashukuru wadau wote kwa kutenga muda wao na kujumuika pamoja katika Futari hiyo kwani kwa kitendo hicho kimeleta faraja na heshima kubwa sana.


Aidha, alisema kuwa, ACB imekuwa na utamaduni wa kufanya hafla ya kufuturisha kwa kila mwaka kwa ajili ya kuunga mkono ndugu zetu Waislam katika funga yao na pia ni njia nzuri ya kuboresha mahusiano ya benki na wateja wake.


Akiba Commercial Bank inatambua na kuheshimu sana Imani za wateja, Wafanyakazi na wadau wake na kuupa umuhimu wa kipekee katika mwezi Mtukufu wa Ramadhan.


Mwisho, Bw. Silvest Arumasi amesema kuwa ACB inaendelea kuboresha na kupanua wigo wa huduma zake ili kuendana na soko kwa lengo ya kukidhi matarajio ya wateja, amewaomba wateja na umma kwa ujumla kuendelea kuiamini Benki hiyo ambayo imeweza kuwahudumia Watanzania wengi na kuleta maendeleo makubwa kwa wajasiriamali na Jamii nzima kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment