Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akikabidhi cheti maalum kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Commercial Bank (TCB), Adam Mihayo mmoja ya wadhamini wa mashindano ya Ligi ya Mapinduzi Cup ikiwa ni kutabua na kuthamini uwepo wa wadhamini mbalimbali na wadau wa michezo.Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Commercial Bank (TCB), Adam Mihayo (kushoto), akikabidhi zawadi ya shilingi 1,000,000/- kwa Mlinda Mlango bora wa mashindano ya Kombe la Mapinduzi Cup 2023/2024 kutoka Timu ya Mlandege, Athuman Hassan, mara baada ya Timu hiyo kuibuka kidedea kwa kuikanda timu ya Simba SC kwa bao 1-0 wakati wa mchezo wa fainali wa kombe hilo. Mchezo huo umefanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya New Amani vilivyopo visiwani Zanzibar na mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mh. Hussen Mwinyi.
Tanzania Commercial Bank PLC (TCB) ambae ni Moja ya wadhamini wa mashindano ya ligi ya Mapinduzi Cup yanayofanyika visiwani Zanzibar kila mwaka Jumamosi iliyopita Benki hiyo ilikabidhi zawadi ya pesa kiasi cha shilingi milioni moja kwa golikipa bora wa ligi hiyo, Athuman Hassan kutoka klabu ya Mlandege FC. Makabidhiano ya zawadi hiyo yalifanyika muda mfupi baada ya kumalizika kwa mchezo wa fainali baina ya Mlandege FC na Simba SC uliofanyika katika Uwanja wa New Amani Visiwani Zanzibar ambapo mchezo ulikamilika kwa timu ya Mlandege kuibuka na ushindi wa Goli 1-0.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi zawadi hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Commercial Bank (TCB), Adam Mihayo amesema TCB itaendelea kutoa hamasa kwenye michezo mbalimbali hapa Nchini kwani michezo imekuwa ikiwakutanisha watu karibu pia michezo ni ajira.
“Zawadi hii tunazitoa kwa kuleta hamasa kwa wachezaji ili wafanye vizuri na kujitangaza kimataifa, pia kusaidia kuboresha mchezo huu mwanzo tu kwa Tanzania Commercial Bank kushiriki katika michezo wa soka hapa nchini” amesema Mihayo.
Tanzania Commercial Bank tumekuwa na utaratibu wa kujitolea sana katika jamii kwa kufauata misingi ya Benki yetu. Tumeweza kusaidia sehemu mbalimbali Tanzania bara pamoja na visiwani katika sekta mbalimbali ikiwepo elimu, afya, michezo, biashara na kutoa elimu ya kifedha.
Hapa visiwani Zanzibar tumeshafanya mambo kadhaa ikiwepo kusaidia vikundi vya wanawake wajasiriamali kwa kuwapa vitendea kazi vikiwemo vyerehani na kuwawezesha vikundi vya kinamama wa Jimbo la Paje wanaolima zao la mwani kwa kuwajengea kisima Cha furahia ili kuwarahisishia shughuli zao za kilimo wa zao hilo ”
“Kwa upande wake Golikipa wa Mlandege Athuman Hassan alishukuru kupata zawadi hiyo na kuahidi kuwa atazidi kuongeza bidii kuwa kinara na kusaidia timu yake kupata ushindi wa kila mechi. “Napenda kuwashukuru TCB kwa kunipa zawadi hii kwani itakwenda kuongeza sana hamasa upande wangu na wa wachezaji wote na makocha pia.
No comments:
Post a Comment