Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Monday, 11 December 2023

TANZANIA ENERGY COOPERATION SUMMIT 2024


Ikiwa ni mojawapo ya eneo lililopendekezwa zaidi kuwa thabiti na muhimu kwa shughuli za uwekezaji barani, Tanzania inajiandaa kuwa mwenyeji wa mkutano wa tano wa mwaka wa kimataifa wa Tanzania Energy Cooperation Summit (TECS) utaofanyika kuanzia Januari 31 mpaka Februari mosi, 2024 jijini Arusha, nyumbani kwa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC)

Dar es Salaam - Desemba 11, 2023: Wawekezaji kutoka sekta mbalimbali, fedha na serikali zitakutana kuonyesha uwezo ilionao Tanzania. Uwezo ambao unaonyeshwa na nchi ambayo kwa sasa imeorodheshwa kuwa ya tatu kusini mwa Jangwa la Sahara kwa uwekezaji siku za mbeleni, ambapo inatarajiwa kuona ukuaji wa Pato la Taifa kwa 6% ifikapo 2025, huku ikishuhudia mamia ya mamilioni, kama sio mabilioni, ya uwekezaji wa dola, unaolenga kuelekezwa kwenye miundombinu, umeme wa maji, gesi asilia (LNG) na miradi ya nishati ya jua katika miaka ya hivi karibuni.

Ikiwa imeorodheshwa na KPMG ikiwa nyuma ya nchi za Afrika ya Kusini na Nigeria, Tanzania imejithibitishia hadhi yake yanapokuja masuala ya biashara na uwekezaji.

Taifa lilitajwa kwa eneo lake la kimkakati mashariki mwa bara la Afrika, wingi wa maliasili, na ongezeko la uwekezaji hivi karibuni, haswa katika sekta ya nishati. Kiwanda cha kwanza cha umeme wa jua cha 50MW kwenye gridi ya taifa, uwekezaji wa dola za Marekani milioni 300 katika nishati ya maji, mradi wa gesi asilia wa dola bilioni 42 ulioanzishwa na Shell, Equinor na Exxon Mobil, na takribani dola za Marekani bilioni 7 zilizoingizwa kwenye miundombinu, inathibitisha mvuto wake barani Afrika na kimataifa.

Ukiwa umeratibiwa na EnergyNet, mkutano wa kimataifa wa TECS24 hautoainisha mafanikio haya ya kujivunia pekee bali itaangazia fursa zijazo za biashara na miradi ya uzalishaji inayotarajiwa kubadilisha nchi na ukanda huu zaidi. Changamoto zinazohusiana na fedha na dhamana pia zitajadiliwa, ili kuchochea ari zaidi ya majadiliano na kuhakikisha sekta ya umeme nchini inaendelea kuimarika zaidi.

Pamoja na wawekezaji wakubwa, wadau watakaohudhuria ni pamoja na mawaziri wa kitaifa kutoka Tanzania, Malawi, na Ethiopia, pamoja na viongozi wa makampuni ya utoaji huduma ya kitaifa, ikiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO wa Tanzania, Gissima Nyamo-Hanga. Wasemaji kutoka Electricidade de Moçambique (EDM) na ZESCO ya Zambia pia watakuwepo. Wao, pamoja na wawakilishi kutoka sekta za umma na binafsi, wakurugenzi kutoka taasisi za kifedha - ikiwa ni pamoja na AfDB, BII, World Bank Group na ATIDI - na mashirika ya kikanda, wote watakuwepo Arusha, kwa ajili ya mkutano wa biashara wa hadhi ya juu wa aina yake.

Kwa kuzingatia nafasi ya Tanzania kama mhimili wa nishati kikanda, mada zitakazojadiliwa ni pamoja na mtazamo wa kiuchumi wa Tanzania na uwezo wa maendeleo ya nishati, pamoja na kupanga njia bora ya kujenga soko la umeme la kikanda. Ushirikiano wa sekta za umma na binafsi katika miradi ya usafirishaji pia utakuwa kwenye ajenda, pamoja na wakurugenzi kutoka taasisi za kifedha, utawala na kanuni, na nafasi muhimu ya nishati mbadala. Washiriki watapewa fursa ya kutoa mawazo kuhusu kutengeneza uunganisho bora wa kikanda, mifumo imara zaidi kwa biashara na uwekezaji, na hatimaye kuunda ramani ya ufikiaji wa nishati kikanda kwa siku za usoni.

"Tanzania imejitengenezea nafasi muhimu kwa biashara barani. Kwa kuwa na uhusiano baina ya kusini na mashariki na pia ulimwenguni kote, nchi hii siku zote imekuwa na uwezo wa kuwa mwanzilishi wa ukuaji wa viwanda - na sasa tunashuhudia jinsi adhma hii itakavyotimizwa. Hivyo nina shauku kubwa kuonyesha ukuaji wa Tanzania kuhakikisha fursa na kasi hii inaendelea," alisema Simon Gosling, Mkurugenzi Mtendaji, EnergyNet.

Aliongeza, "Pia tunafurahi kuandaa mkutano huu Arusha, ukitoa muda na nafasi kwa kila mtu kujadili kwa kina masuala muhimu zaidi kuhus sekta mbalimbali."

"Tanzania akiwa mmojawapo wa nchi waanzilishi wa Jumuiya yetu, tuna nia ya dhati kuiunga mkono zaidi kusaidia malengo yake kwenye sekta ya nishati. Tukiendeleza mafanikio yaliyopatikana katika mkutano wa mwaka jana uliofanyika Dar es Salaam, tunatumaini kuwa TECS24 itatoa ufafanuzi zaidi kuhusu nafasi ya sekta binafsi katika sekta ya nishati na jinsi wakurugenzi kutoka taasisi za kifedha - hasusani watoaji wa bima na dhamana wa kikanda kama vile ATIDI - wanaweza kusaidia juhudi hizo na mabadiliko makubwa ya nishati kwa ujumla," alisema Obbie Banda, Mchambuzi na Kaimu Mratibu wa Regional Liquidity Support Facility (RLSF) katika taasisi ya African Trade and Investment Development Insurance (ATIDI).

Aleem Tharani, Mkuu mwenza wa Infrastructure Sector Group (Afrika), Bowmans na Mkuu wa Miradi, Nishati na Miundombinu (Afrika), alihitimisha: "Mkutano wa 5 wa kimataifa wa Tanzania Energy Cooperation Summit unaweka alama muhimu kwa sekta ya nishati barani Afrika. Kwa kuwaunganisha wawekezaji, taasisi za serikali na wataalamu wa sekta, tunachochea majadiliano muhimu kwa ajili ya kukuza ramani ya nishati ya Tanzania, kutoa kipaumbele kwa gesi na nishati mbadala, na kuboresha usafirishaji wa kikanda. Bowmans inajivunia kudhamini mkutano huu, ikiona umuhimu wake katika kuunda mustakabali wa nishati wa Afrika na kuzidisha ushirikiano wa umma na binafsi."

Angalia ajenda na orodha ya wasemaji hapa https://www.tanzania-ecs.com/

About EnergyNet

FACILITATING ENERGY INVESTMENT IN FAST-GROWING ECONOMIES - EnergyNet has produced investment forums and executive dialogues for Africa and Latin America's power sectors for the last 25 years - in Europe, the USA, Asia and across Africa and Latin America.

We work with governments and national utilities to facilitate investment summits where credible international investors can build relationships with public sector stakeholders to advance access to power.

Best known for the Africa Energy Forum, the longest-serving business development meeting place for senior-level decision makers in Africa's power sector, other leading investment summits we provide strategic perspectives on the investment landscape and project preparation include the Tanzania Energy Cooperation Summit, H2 Africa, Offshore Technology Africa, Powering Africa Summit, Latin American Energy Forum and Latin American & Caribbean Gas Conference and Exhibition. YES! Youth Energy Summit and YES! Youth Energy Day are part of the portfolio, with a focus on creating a platform and network to boost the skills, connections and business readiness of a new generation of African energy leaders

Having this focus on public and private sector partnerships provides us with a valuable lens through which we can offer independent perspectives and support the business development activities of companies from around the world operating in these fast-growing markets. Our team talks daily with stakeholders across Africa, Latin America and the Caribbean to support these insights, so relationships and investor insights are our business and our passion.

Headquarters: London, UK

For further information, please visit our website https://energynet.co.uk/

No comments:

Post a Comment