Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Thursday, 16 November 2023

TANGA CEMENT NA TWIGA CEMENT KUUNGANISHWA


Mwenyekiti wa bodi wa kampuni ya Tanga cement PLC, Patrick Rutabanzibwa (katikati), akizungumza wakati wa mkutano mkuu wa mwaka na mkutano maalum wa wanahisa wa kampuni hiyo uliofanyika jijini Dar es salaam. Wengine ni Mkuu wa Divisheni ya Fedha wa Tanga Cement PLC, Pieter De Jager (kushoto) Mkurugenzi Mtendaji wa Tanga Cement PLC, Reinhardt Swart (wa pili kulia) na Raymond Mbilinyi, mmoja wa wakurugenzi wa bodi ya Tanga Cement pamoja na Katibu wa kampuni ya Tanga Cement, Quresh Ganijee.



Mkurugenzi Mtendaji wa Tanga Cement PLC, Reinhardt Swart (wapili kushoto), akizungumza wakati wa mkutano mkuu wa mwaka na mkutano maalum wa wanahisa wa kampuni hiyo uliofanyika jijini Dar es salaam Wengine ni Mkuu wa Divisheni ya Fedha wa Tanga Cement PLC, Pieter De Jager (kushoto) Mwenyekiti wa bodi ya Tanga cement, Patrick Rutabanzibwa, (wa tatu kulia) na Raymond Mbilinyi, ambaye ni mmoja wa wakurugenzi wa bodi wa Tanga Cement na Katibu wa kampuni ya Tanga Cement Quresh Ganijee.


Baraza la ushindani nchini FCT limeridhia mchakato wa uunganishaji kampunu ya saruji ya tanga na ile ya twiga huku wanahisa wa kampuni ya saruji ya tanga nao wakipitsha maamuzi ya kuruhusu uuzaji hisa asilimia 73 za kampuni hiyo kwenda kwa mwekezaji heidberg ambaye ndiye mmiliki kiwanda cha twiga cement.

Maamuzi hayo yamepitishwa jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano mkuu wa mwaka na mkutano maalum wa wanahisa hisa wa kampuni ya saruji ya tanga Cement ambapo akizungumza Mwenyekiti wa bodi wa kampuni hiyo, Patrick Rutabanzibwa amesema maamuzi ya wana hisa hao yametokana na hali ngumu inayo ipitia kampuni ya Tanga Cement ambayo imeshindwa kutoa gawio kutokana na deni ambalo lipo kwenye kampuni hiyo.

Kampuni hiyo pia ilielemewa na gharama kubwa za uzalishaji hivyo kujikuta wakihitaji zaidi uwekezaji kutoka kampuni ya heidelberg inayo miliki kampuni ya scancem ambaye ndie mmiliki wa kiwanda cha twiga cement ili kuingiza nguvu nakuhakikishia wateja kuwa na uhakika wakupata bidhaa hiyo bila kuwa na mashaka.

Kwa upande wake mmiliki wa kampuni ya african mauritus ambaye anamiliki hisa zaidi ya asilimia 73 ya kiwanda cha Tanga Cement, Reinhardt Swart ambaye ndie Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha Tanga Cement amesema mchakato wa upatikanaji wa mwekezaji huyo utakamilika haraka iwezekanavyo ili kuongeza nguvu ya uzalishaji wa saruji ambapo pia ameiomba serikali kuimarisha upatikanaji wa nishati kwa uhai wa viwanda nchini.

Hata baadhi ya wana hisa wa kiwanda cha Tanga Cement ambao wameeleza kusikitishwa na kukosa gawio kwa muda mrefu huku wakibariki kuuzwa kwa hisa hizo na kuunganishwa kwa kiwanda cha tanga cement na twiga cement ili kuwa kiwanda kimoja kitakacho kuwa imara.

No comments:

Post a Comment