Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Friday 24 November 2023

MTEJA WA Y9 MICROFINANCE AJISHINDIA PIKIPIKI

Mkurugenzi wa Mauzo na Usambazaji wa Taasisi ya Kifedha Y9 Microfinance, Fredrick Mtui (katikati) akizungumza na mshindi wa pikipiki droo ya saba kwa njia ya simu Anorld Jacob na Jekapo ambaye amejishindia simu janja wote ni wakazi wa Dar es Salaam ikiwa ni muendelezo wa Y9 kutoa zawadi kila wiki Kwa wateja wake. Hafla ya kuchezesha droo hiyo imefanyika leo jijini Dar es salaam, Wengine pichani ni Meneja Masoko ya Taasisi hiyo Bi. Sophia Mang'enya pamoja na mshindi wa pikipiki Wa droo ya sita Bw Baraka Bazarae (kushoto).
Meneja Masoko ya taasisi, Bi. Sophia Mang'enya akimkabidhi zawadi ya pikipiki mmoja kati ya washindi wa droo ya sita Baraka Bazarae katika hafla ya uchezeshwaji wa droo ya saba iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mshindi wa pikipiki Droo ya sita ya Y9 Microfinance Baraka Bazarae Katikati akizungumza wakati wa hafla ya kuchezesha droo ya saba iliyofanyika leo jijini Dar es salaam, Wengine pichani Mkurugenzi wa mauzo na usambazaji wa taasisi ya kifedha Y9 microfinance, Fredrick Mtui (kulia) na Mkaguzi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha nchini, Salim Buguvi (kushoto).

Meneja Masoko ya Taasisi ya Kifedha ya Y9 Microfinance, Bi. Sophia Mang'enya (kulia), akimkabidhi zawadi ya pikipiki kwa mshindi wa droo ya sita, Baraka Bazarae ambae aliibuka kidedea wakati wakuchezesha droo ya sita wiki iliyopita makabidhiano hayo yalifanyika wakati wa yakuchezesha droo kwaajili ya kutafuta washindi wa droo ya Saba. Kushoto ni Mkaguzi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha nchini, Salim Buguvi (kushoto).

Washindi wa Droo ya saba ya Y9 Microfinance wapatikana mshindi wa pikipiki ni Anorld Jacob na mshindi wa simu Jekapo wote wakiwa ni wakazi wa Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa kuchezesha droo hiyo Mkurugenzi wa mauzo na usambazaji taasisi ya kifedha Y9 microfinance, Fredrick Mtui ameeleza kuwa huu ni muendelezo wa Y9 microfinance kuchezesha droo kila wiki na kupata washindi wawili.

Alisema "Matamanio makubwa ya Y9 microfinance ilikuwa ni kuhakikisha kuwa kila mteja wa Y9 microfinance anapata nafasi ya kushiriki na kushinda katika droo inayochezeshwa kila wiki.

No comments:

Post a Comment