Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Friday, 24 November 2023

ECOBANK YASHIRIKI WIKI YA HUDUMA ZA FEDHA ARUSHA

Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Ecobank, Furaha Samalu (kulia) akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella.

Ecobank imeshiriki katika Maonyesho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kimataifa yaliyoandaliwa na Wizara ya Fedha.

Maonyesho hayo yanafanyika Arusha kuanzia Tarehe 20 mpaka 26 November 2023 katika uwanja wa Sheikh Abeid Karume na yalifunguliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Yakima na Kauli mbiu "Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi".

Ecobank; Bank ya Kiafrika iliyopo katika nchi zaidi ya 33 Barani Africa; inatoa huduma bora na za kisasa za kibenki.

Fanya malipo kiurahisi kupitia simu ya kiganjani BUREEEEE! Lipia King'amuzi, Luku, bili za maji, na vinginevyo kwa kutumia Ecobank Mobile app.

Ecobank inakupatia Huduma za mikopo mbalimbali kwa wafanyakazi na wafanya biashara wakubwa, wakati na wadogo.

Ecobank ina matawi na mashine za kutolea fedha (ATMs) machines katika maeneo mbalimbali jijini Dares Salaam, Mwanza na Arusha.

Fungua akaunti na Ecobank leo ufurahie huduma za kibenki kiganjani mwako kwa kutumia Ecobank Mobile App.

Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Ecobank bi Furaha Samalu amesema Benki hiyo inayofuraha kushiriki katika Maonyesho hayo ilikupata nafasi ya kuwaelimisha wananchi wa Arusha na vitongoji vyake huduma za kibenki zitolewazo na Benki ya Ecobank.

Tembelea Banda La Ecobank lililopo uwanja wa Sheikh Abeid Karume kupata elimu ya Fedha na jinsi ya kupata mitaji kuendeleza biashara zako.

Tawi la Ecobank Arusha lipo katika jengo la Mafao barabara ya Nyerere kupata Huduma bora na za kisasa za kibenki.

No comments:

Post a Comment