Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday 28 November 2023

EACOP YAKABIDHI FIDIA NYUMBA YA 339 MKOANI TANGA


Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki - sehemu ya Tanzania leo imekabidhi nyumba ya 339 ambayo ni ya mwisho katika utaratibu wa kuwalipa fidia wananchi waliopitiwa na mradi huo kubwa wa bomba la mafuta.


Mpango wa nyumba mbadala, unaojumuisha jumla ya nyumba 339 pamoja na miundo mbinu yake midogo , imekuwa msingi wa dhamira yetu kwa kaya zilizoguswa na mchakato wa utwaaji ardhi.


EACOP tayari imekabidhi jumla ya nyumba 339 kwa Watu 293 walioguswa kwa kupoteza makazi yao katika Mikoa 8 ya Kagera, Geita, Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma, Manyara na Tanga; ikijumuisha Wilaya 21 na Vijiji 1,02I. Kati ya nyumba mbadala hizo 339 na miundo mbinu yake midogo, Nyumba mbadala 43 zilikabidhiwa kwa waguswa 30 walioguswa na utwaaji wa ardhi wa awali kwa ajili ya kambi kuu na yadi za mabomba mwaka 2022 katika Wilaya za Missenyi, Muleba, Bukombe, Nzega na Singida. Nyumba mbadala 296 zilikuwa kwa ajili ya kaya zilizoguswa na utwaaji wa ardhi wa kwa ajili ya mkuza wa bomba wenye urefu wa kilomita 1,143 unaokatiza katika mikoa 8.


Akiongea wakati wa makabidhiano ya nyumba ya mwisho mkoani Tanga, Meneja Mkuu wa EACOP Tanzania Wendy Brown alisema ujenzi wa nyumba hizi ulifanywa na wakandarasi wa ndani walioajiri watu kutoka jamii za wenyeji, na kuhakikisha dhamira ya EACOP ya ushirikishwaji wa jamii za wenyeji na maendeleo endelevu. Makabidhiano ya nyumba mbadala za mwisho yanahitimisha safari ndefu ya mchakato wa utwaaji wa ardhi kwa ajili ya Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki - sehemu ya Tanzania.

“Nchini Tanzania, waguswa 344 kati ya 9,904 walipoteza makazi, na kati ya hao 293 walichagua nyumba mbadala ikiwa ni pamoja na miundo mbinu yake midogo kama aina yao ya fidia. Ujenzi wa nyumba mbadala ulizingatia ushirikishwaji wa dhati wa waguswa, mchakato wa uthamini, utoaji wa wazi wa taarifa, na maelezo ya ana kwa ana juu ya vifurushi au aina za fidia kabla ya kusaini mikataba ya fidia. Nyumba mbadala zimejengwa kwenye ardhi iliyonunuliwa na Mradi na TPDC au ardhi ya mguswa ilyopo. Ramani ya jengo ilichorwa kutegemea upendeleo wa mguswa na mwongozo wa kiufundi kutoka EACOP,” alisema

Kama sehemu ya kifurushi cha nyumba mbadala kila mguswa alipewa nyumba mbdala ikiwa ni pamoja na tanki la maji la lita 5000 pamoja na safu ya umeme wa jua ya wati 400, yenye na betri ya ampia 200 za masaa ya mkondo wa umeme, inveta na kifaa cha kudhibiti chaji.

Nyumba mbadala zote zina waranti ya kipindi cha mwaka mmoja. Katika kipindi hiki, mradi utawajibika kwa matengenezo ya kasoro zozote katika nyumba mbadala kupitia kwa wakandarasi wake.

Waguswa wanaostahiki (hasa walio katika mazingira magumu) hupatiwa msaada wa mpito (vikapu vya chakula), usaidizi wa uhamisho (ili kuwasaidia kusafirisha mali zao hadi eneo jipya) na upatikanaji wa programu za urejeshaji wa ustawi wa maisha, unaolenga kurejesha ustawi na viwango vya maisha.

Mpango wa nyumba mbadala ni sehemu muhimu ya shughuli za EACOP unaohusisha ujenzi na uendeshaji wa bomba la chini ya ardhi, linalokatisha mipaka ya nchi mbili. Bomba hili lililoundwa ili kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani Tanga linawakilisha maendeleo makubwa katika miundombinu ya nishati ya kikanda. Dhimira ya EACOP katika mpango wa ujenzi wa nyumba mbadala inaoneonekana katika dhamiara yake ya uvumbuzi, mazingira na uwajibikaji wa kijamii.

Katika kuonyesha wajibu wa EACOP wa kuendeleza watoa huduma wa ndani, ujenzi wa nyumba hizi ulikabidhiwa kwa wakandarasi watatu wa ndani (3) wenye ujuzi ambao ni SBS Limited, VJ Mistry na CF Builders. Imechukua miezi 15 tangu kuanza kwa ujenzi mpaka kukamilika kwake. Mbinu hii sio tu ilihakikisha ujenzi wenye ubora zaidi lakini pia ilichangia maendeleo ya kiuchumi kwa kukuza wajasiriamali wa ndani.

Mpango huu wa ujenzi umeleta manufaa makubwa kwa wanajamii walio na wanaozunguka Muheza katika Mkoa wa Tanga. Jamii za wenyeji zilishiriki kikamilifu katika mchakato wa ujenzi, na kuchangia mafanikio ya kukamilika kwake, na wakati huo huo kujenga uwezo wao wa kazi za mikono. Hii inachangia uendelevu na kuwapa wanajamii ujuzi muhimu.

Mpango wa nyumba mbadala umetoa fursa za ajira za muda mfupi kwa jamii za wenyeji. Kwa kushirikiana na wakandarasi wa ndani na kuajiri wanajamii, EACOP iliingiza rasilimali katika uchumi wa eneo hilo, na hivyo kukuza hali ya fahari ya umiliki miongoni mwa wafanyakazi.

Meneja Mkuu wa EACOP Wendy Brown, Tawi la Tanzania anasema kuwa "Kukamilika kwa mpango wa ujenzi wa nyumba mbadala kunaonyesha dhamira ya EACOP katika viwango vya fedha vya kimataifa vya mchakato wa utwaaji ardhi. Tunajivunia kushirikiana na wakandarasi wa ndani katika mchakato wa ujenzi, kuiwezesha jamii tunayohudumia na kuhakikisha majengo yenye ubora wa juu zaidi kwa wale walioguswa na mradi wa bomba."

"Kufanya kazi na VJ Mistry, SBS na CF Builders kwenye mpango huu imekuwa mchakato wenye ushirikiano wa kweli. Dhamira ya EACOP ya kushirikisha wakandarasi wa ndani sio tu imechangia katika mafanikio ya programu bali pia pia fursa za kiuchumi kwa jamii."

No comments:

Post a Comment