Daktari kutoka timu ya Afya Check, Dkt. Elias Joseph (kushoto) akizungumza na mmoja wa wakazi wa Mwanza waliojitokeza kupata ushauri na matibabu ya bure yanayoendeshwa na msafara wa Twende Butiama katika viwanja vya Furahisha jijini humo. Msafara huu ambao umedhaminiwa na asasi ya Vodacom Tanzania Foundation unajumuisha waendesha baiskeli takribani 200 walioanza safari jijini Dar es Salaam Oktoba mosi na wanatarajia kufika Wilayani Butiama Oktoba 14 ikiwa ni juhudi za kuenzi maisha na urithi wa Mwalimu Nyerere kupitia utekelezaji wa shughuli za elimu, mazingira na afya. |
No comments:
Post a Comment