DAR ES SALAAM, Oktoba 22, 2023 - Kwa mara ya kwanza nchini Tanzania, Serengeti Lite Oktobafest ilileta pamoja vipaji vya muziki na ubunifu wa hali ya juu wa Afrika Mashariki katika fukwe za Dar es Salaam, ikitoa burudani na kuonyesha utamaduni. Tukio hili la kipekee lilijumuisha safu ya wasanii maarufu, ikiwa ni pamoja na Nyanshiski kutoka Kenya, Jose Chameleon kutoka Uganda, Ali Kiba, Bill Nas, Chino, G Nako, na wabunifu kama vile Makeke International kutoka Tanzania, wote wakishirikiana kwenye jukwaa moja kugusa mioyo ya maelfu ya Waafrika Mashariki.
Pamoja na hayo, usalama ulikuwa ni kipaumbele cha juu, huku waandaaji wa tamasha wakishirikiana na Uber, wakitoa punguzo la asilimia 40 kwa watu wanaenda kwenye tamasha kwa safari za kwenda na kurudi Coco Beach. Hatua hii ililenga kuzuia hatari zinazohusiana na uendeshaji wa magari wakiwa wamelewa, kuhakikisha kuwa washiriki wote walikuwa na njia salama na ya kuaminika ya usafiri.
Vipaji vilivyoonyeshwa katika jukwa la Serengeti lite vilikua ni vya kipekee na hakika watu waliburudika na aonyesho ya wasanii yaliyogusa mioyo ya hadhira na kudhirisha utajiri wa tofauti za kitamaduni za Afrika Mashariki.
Kuhusu SBL:
Ilianzishwa mwaka 1988 kama Associated Breweries, SBL ni kampuni ya pili kwa ukubwa nchini Tanzania, na chapa zake za bia zilichukua nafasi ya Zaidi ya 25% ya soko kwa ujazo. SBL ina mitambo mitatu ya uendeshaji iliyopo Dar es Salaam, Mwanza na Moshi.
Tangu kuanzishwa kwa SBL mwaka 2002 biashara hiyo imekuza jalada lake la chapa mwaka hadi mwaka. Upatikanaji wa hisa nyingi na EABL/Diageo mwaka 2010 umeongeza uwekezaji katika viwango vya ubora wa kimataifa na kusababisha nafasi kubwa za ajira kwa watu wa Tanzania. Chapa za SBL zimepokea tuzo nyingi za kimataifa zikiwemo Serengeti Premium Lager, Serengeti Lite, Pilsner Lager, Guinness Stout, na Guinness Smooth. Kampuni hii pia ni nyumbani kwa vinywaji vikali duniani kama vile Johnniew Walker Whisky, Smirnoff Vodka, Gordon’s Gin, Captain Morgan Rum, Baileys Irish Cream, na chapa zinazozalishwa nchini kama vile Bongo Don SBL’S maiden local spirit brand na Smirnoff Orange.
Kwa maelezo zaidi wasiliana na:
Rispa Hatibu,
Meneja Mawasiliano na Uendelevu wa SBL,
Simu: +255 685 260901
Barua Pepe: Rispa.Hatibu@diageo.com
No comments:
Post a Comment