Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Monday 2 October 2023

TWENDEBUTIAMA YAANZA SAFARI YA KILOMETA 1,500 KUTOKA DAR ES SALAAM KUELEKEA BUTIAMA

Mjane wa Hayati Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere akizungumza na washiriki wa msafara wa waendesha baiskeli wa Twende Butiama na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi rasmi wa kuanza kwa safari yao ya kutoka Dar es Salaam, Oktoba mosi, kuelekea Wilaya ya Butiama ambapo wanatarajia kufika Oktoba 14. Wakimsikiliza wa kwanza kushoto ni Meneja Michezo wa Baraza la Michezo la Taifa, Bw. Benson Chacha aliyemwakilisha Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro, akifuatiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Bw. Philip Besiimire, pamoja na Mwenyekiti wa bodi ya Vodacom Tanzania Foundation, Bi. Harriet Lwakatare (wa kwanza kulia). Waendesha baiskeli takribani 200 watasafiri kwa kilometa zaidi ya 1,500 na kupita kwenye wilaya 20 ndani ya mikoa 10, kuenzi maisha na urithi aliotuachia Mwalimu Nyerere kwa kujihusisha na shughuli za elimu, afya, na mazingira wakiwa njiani.

Mwenyekiti wa bodi ya Vodacom Tanzania Foundation, Bi. Harriet Lwakatare akizungumza na washiriki wa msafara wa waendesha baiskeli wa Twende Butiama na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi rasmi wa kuanza kwa safari yao ya kutoka Dar es Salaam, Oktoba mosi, kuelekea Wilaya ya Butiama ambapo wanatarajia kufika Oktoba 14. Wakimsikiliza kutoka kulia ni Mjane wa Hayati Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Bw. Philip Besiimire, pamoja na Meneja Michezo wa Baraza la Michezo la Taifa, Bw. Benson Chacha aliyemwakilisha Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro. Waendesha baiskeli takribani 200 watasafiri kwa kilometa zaidi ya 1,500 na kupita kwenye wilaya 20 ndani ya mikoa 10, kuenzi maisha na urithi aliotuachia Mwalimu Nyerere kwa kujihusisha na shughuli za elimu, afya, na mazingira wakiwa njiani.
Msemaji wa familia ya Mwalimu Nyerere, Waziri Mkuu mstaafu, Joseph Sinde Warioba akizungumza na washiriki wa msafara wa waendesha baiskeli wa Twende Butiama na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi rasmi wa kuanza kwa safari yao ya kutoka Dar es Salaam, Oktoba mosi, kuelekea Wilaya ya Butiama ambapo wanatarajia kufika Oktoba 14. Wakimsikiliza kutoka kulia ni Mwenyekiti wa bodi ya Vodacom Tanzania Foundation, Bi. Harriet Lwakatare, Mjane wa Hayati Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Bw. Philip Besiimire, pamoja na Meneja Michezo wa Baraza la Michezo la Taifa, Bw. Benson Chacha aliyemwakilisha Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro. Waendesha baiskeli takribani 200 watasafiri kwa kilometa zaidi ya 1,500 na kupita kwenye wilaya 20 ndani ya mikoa 10, kuenzi maisha na urithi aliotuachia Mwalimu Nyerere kwa kujihusisha na shughuli za elimu, afya, na mazingira wakiwa njiani.

Meneja Michezo wa Baraza la Michezo la Taifa, Bw. Benson Chacha, aliyemwakilisha Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro, akizungumza na washiriki wa msafara wa waendesha baiskeli wa Twende Butiama na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi rasmi wa kuanza kwa safari yao ya kutoka Dar es Salaam, Oktoba mosi, kuelekea Wilaya ya Butiama ambapo wanatarajia kufika Oktoba 14. Wakimsikiliza kutoka kulia ni Mwenyekiti wa bodi ya Vodacom Tanzania Foundation, Bi. Harriet Lwakatare, Mjane wa Hayati Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere, pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Bw. Philip Besiimire. Waendesha baiskeli takribani 200 watasafiri kwa kilometa zaidi ya 1,500 na kupita kwenye wilaya 20 ndani ya mikoa 10, kuenzi maisha na urithi aliotuachia Mwalimu Nyerere kwa kujihusisha na shughuli za elimu, afya, na mazingira wakiwa njiani.

Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Foundation, Zuweina Farah akizungumza na washiriki wa msafara wa waendesha baiskeli wa Twende Butiama na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi rasmi wa kuanza kwa safari yao ya kutoka Dar es Salaam, Oktoba mosi, kuelekea Wilaya ya Butiama ambapo wanatarajia kufika Oktoba 14. Wakimsikiliza kutoka kulia ni Mwenyekiti wa bodi ya Vodacom Tanzania Foundation, Bi. Harriet Lwakatare, Mjane wa Hayati Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Bw. Philip Besiimire, pamoja na Meneja Michezo wa Baraza la Michezo la Taifa, Bw. Benson Chacha, aliyemwakilisha Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro. Waendesha baiskeli takribani 200 watasafiri kwa kilometa zaidi ya 1,500 na kupita kwenye wilaya 20 ndani ya mikoa 10, kuenzi maisha na urithi aliotuachia Mwalimu Nyerere kwa kujihusisha na shughuli za elimu, afya, na mazingira wakiwa njiani.

Meneja Michezo wa Baraza la Michezo la Taifa, Bw. Benson Chacha, aliyemwakilisha Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (katikati) akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Bw. Philip Besiimire (kushoto) na Mwenyekiti wa bodi ya Vodacom Tanzania Foundation, Bi. Harriet Lwakatare (kulia), mbele ya waendesha baiskeli takribani 200 wa msafara wa Twende Butiama kuashiria kuanza kwa safari yao ya kutoka Dar es Salaam, Oktoba mosi, kuelekea Wilaya ya Butiama ambapo wanatarajia kufika Oktoba 14. Waendesha baiskeli hawa watasafiri kwa kilometa zaidi ya 1,500 na kupita kwenye wilaya 20 ndani ya mikoa 10, kuenzi maisha na urithi aliotuachia Mwalimu Nyerere kwa kujihusisha na shughuli za elimu, afya, na mazingira wakiwa njiani.
Kuelekea kumbukumbu ya kumuenzi baba wa taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye alifariki Oktoba 14, 1999, msafara wa waendesha baiskeli unaojulikana kama Twende Butiama umeanza rasmi safari leo katika makazi yake Msasani jijini Dar es Salaam ambapo unatarajiwa kufikia tamati Oktoba 14, Wilayani Butiama.


Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro, Meneja Michezo wa Baraza la Michezo la Taifa, Bw. Benson Chacha aliwapongeza waandaaji wa Twende Butiama pamoja na wadhamini wa msafara huo, taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation kwa jitihada za kufanikisha tukio hili ambalo linahamasisha Watanzania kupenda michezo, kutunza mazingira na kujali afya zao.


“Nichukue fursa hii kuwapongeza kwa dhati waandaji na washiriki wote wa msafara wa Twende Butiama ambao wana dhamira ya dhati ya kumuenzi baba wa taifa. Tukio hili sio tu linachagiza shughuli mbalimbali ambazo Mwalimu Nyerere alikuwa anazipa kipaumbele lakini pia zitahamasisha Watanzania kupenda michezo. Michezo ni sekta muhimu ambayo ukiachana na kuimarisha afya lakini pia huleta umoja na mshikamano miongoni mwa watu. Pia, niwapongeze Vodacom kwa kudhamini ziara hii ambayo itapita mikoa tofauti ukihamasisha shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii. Mchango wenu kwenye kudhamini sekta ya michezo tunaufahamu na tungependa kuona mkifanya hivyo kwenye michezo mingine kama vile riadha, masumbwi, na kadhalika,” alimalizia Bw. Chacha.

Madhumuni ya msafara huu utakaokuwa na waendesha baiskeli takribani 200 watakaoendesha baiskeli kwa kilometa 1,500 na kupita kwenye wilaya 20 ndani ya mikoa 10, ni kuenzi maisha na urithi aliotuachia Mwalimu Nyerere ambapo alikuwa akipambania kuhusu elimu bora, upatikanaji wa huduma za afya ili kuondokana na maradhi pamoja na ukuaji wa uchumi miongoni mwa Watanzania wote.

Kwa upande wake msemaji wa familia ya Mwalimu Nyerere, Waziri Mkuu mstaafu, Joseph Sinde Warioba alizungumza kwa uchache wakati wa kuanza rasmi kwa msafara wa waendesha baiskeli nyumbani kwa Mwalimu, Msasani jijini Dar es Salaam kwa kusema, “nimefurahi kuona tukio hili limeweza kukusanya nchi tofauti zikiwemo zote za Afrika ya Mashariki kitu ambacho kinaonyesha mshikamano wetu. Njiani mtakapopita mtaweza kujionea nchi yetu ya Tanzania kwa upana wake na kupitia shughuli mtakazozifanya njiani zitawanufaisha Watanzania. Ni matumaini yangu kuwa kupitia msafara wenu mtaweza kuhamasisha mabadiliko kwenye sekta ambazo mtaziangazia kama yalivyokuwa malengo ya Mwalimu. Bado sekta za elimu, mazingira na afya zina mchango mkubwa kwa manufaa ya umma na nimefurahi kuona mmejikita kwenye maeneo haya. Niwatakie kila la kheri muwapo njiani na bila shaka tutajumuika pamoja kuwapokea mtakapofika Butiama.”

Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya Vodacom Tanzania Foundation, Bi. Harriet Lwakatare, ambao ndio wadhamini wakuu wa msafara huo kwa 2023, ameongezea kuwa, “kama tulivyoeleza wakati wa uzinduzi wa ushirikiano wetu, tuna imani kubwa na Twende Butiama hususani kwa kile wanachokifanya katika kuenzi maisha na urithi wa Mwalimu. Elimu, afya, na mazingira ni vipaumbele vikubwa vya taasisi yetu na siku zote tupo mstari wa mbele kushirikiana na wadau wengine kuhakikisha maeneo haya yanaboreshwa ili kuwanufaisha Watanzania sehemu tofauti nchini kote. Ningependa kutoa wito kwa Watanzania wote kuendelea kuunga mkono kampeni ya kuchangia dawati inayoendelea kupitia LIPA NAMBA 5483454, na kujumuika nasi katika shughuli za upandaji miti, na kushiriki kwenye kambi ya bure ya matibabu tutakayoiendesha.”

Kwa kumalizia Mwenyekiti wa Twende Butiama, Bw. Gabriel Landa amesema kuwa, “baada ya kuwatangazia Watanzania uwepo wa msafara wa Twende Butiama takribani wiki mbili zilizopita, hatimaye ile siku tuliyokuwa tunaisubiria kwa hamu imefika. Leo Oktoba mosi tukiwa hapa na washiriki takribani 200, tumeanza safari yetu kutokea nyumbani kwa Mwalimu, Msasani jijini Dar es Salaam na tunatarajia kufika Wilayani Butiama Oktoba 14. Tunawashukuru wadhamini wakuu wa mwaka huu, taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation, wadau, na Watanzania kwa ujumla wanaozidi kutuonyesha ushirikiano wao. Tukiwa njiani tutajihusisha na shughuli za kupanda miti, kuchangia madawati kwa shule za msingi za umma kwenye mikoa tofauti. Pia, tunawaomba watu wajitokeze kwa wingi kutuunga mkono njiani katika njia tutakazopita na kututia moyo.”

No comments:

Post a Comment