Mkuu wa chuo hicho, Isaya Kigava akizungumza katika hafla hio iliyofanyika katika chuo cha Mtakatifu Maria Goretti, Iringa. |
Mkurugenzi Masuala ya Umma wa SBL, John Wanyancha akizungumza katika hafla hio iliyofanyika katika chuo cha Mtakatifu Maria Goretti, Iringa. |
Sharifa Nuhu Maketa, mmoja wa wanufaika wa zamani wa programu hio akizungumza katika hafla hio iliyofanyika katika chuo cha Mtakatifu Maria Goretti, Iringa. |
Mwananfunzi mpya wa programu hio, Annastazia Koko akizungumza katika hafla hio iliyofanyika katika chuo cha Mtakatifu Maria Goretti, Iringa. |
Iringa, (19/10/2023) – Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) imetangaza kundi lingine la wanafunzi wanaofadhiliwa kupitia programu yao ya Kilimo Viwanda, inayolenga kutoa fursa ya elimu kwa wanafunzi wasio na uwezo wanaosoma kozi za kilimo.
Katika miaka minne iliyopita, Programu ya Kilimo Viwanda imesaidia zaidi ya wanafunzi 300 katika harakati zao za kusomea kozi ya kilimo, huku ikijenga mfumo endelevu wa wataalamu wenye ujuzi ambao wanachangia kwa kiasi kikubwa katika maendeleo ya kilimo nchini Tanzania.
Akizungumza katika tafrija ya kutoa ufadhili wa masomo, Mkurugenzi Mtendaji wa Serengeti Breweries, Obinna Anyalebechi alisema, “Ufadhili huu ni sehemu ya ahadi yetu ya kusaidia maendeleo ya kilimo nchini. Tunaamini kuwa program hii itasaidia sana kuimarisha rasilimali ya wataalamu wa kilimo nchini kwa kusaidia wakulima kuongeza uzalishaji na hatimaye mapato”.
Mkurugenzi alisema kwamba mwaka huu, SBL itawasaidia wanafunzi wapya watano ambao watajiunga na wanafunzi tisa ambao tayari wanasomea taaluma za kilimo katika Shule ya St. Maria Goretti huko Iringa. Upanuzi huu wa program unaonyesha dhamira ya Serengeti Breweries ya kusaidia utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya sekta ya kilimo, lengo kuu likiwa kuongeza uzalishaji na mapato ya wakulima.
Mkurugenzi wa Mnyororo wa Ugavi wa Serengeti Breweries, Bw. Alfred Balkagira pia alisifu, “Programu hii inachochea vipaji vya ndani, ikiongeza uwezo wa upatikanaji wa malighafi za ndani. Hatua hii sit u inapunguza gharama bali pia inachangia kwa kiasi kikubwa katika ukuaji wa jamii za wakulima zinazozunguka, ikijenga uhusiano thabiti kati ya SBL na jamii ya eneo hilo”.
Zaidi ya hayo, wanafunzi wanaosoma kupitia program hii huenda wakawa mabingwa wa mbinu endelevu za kilimo, na hivyo kuathiri kwa njia chanya mchakato wa upatikanaji na uzalishaji. Dhana zao mpya na mawazo ya ubunifu zitasaidia kuongeza ufanisi na kusawazisha upatikanaji wa malighafi za SBL kutoka kwa wakulima kwa ajili ya uzalishaji wa bia, kama shayiri, mahindi na mtama.
Kuhusu SBL:
Ilianzishwa mwaka 1988 kama Associated Breweries, SBL ni kampuni ya pili kwa ukubwa nchini Tanzania, na chapa zake za bia zilichukua nafasi ya Zaidi ya 25% ya soko kwa ujazo. SBL ina mitambo mitatu ya uendeshaji iliyopo Dar es Salaam, Mwanza na Moshi.
Tangu kuanzishwa kwa SBL mwaka 2002 biashara hiyo imekuza jalada lake la chapa mwaka hadi mwaka. Upatikanaji wa hisa nyingi na EABL/Diageo mwaka 2010 umeongeza uwekezaji katika viwango vya ubora wa kimataifa na kusababisha nafasi kubwa za ajira kwa watu wa Tanzania. Chapa za SBL zimepokea tuzo nyingi za kimataifa zikiwemo Serengeti Premium Lager, Serengeti Lite, Pilsner Lager, Guinness Stout, na Guinness Smooth. Kampuni hii pia ni nyumbani kwa vinywaji vikali duniani kama vile Johnniew Walker Whisky, Smirnoff Vodka, Gordon’s Gin, Captain Morgan Rum, Baileys Irish Cream, na chapa zinazozalishwa nchini kama vile Bongo Don SBL’S maiden local spirit brand na Smirnoff Orange.
Kwa maelezo zaidi wasiliana na:
Rispa Hatibu,
Meneja Mawasiliano na Uendelevu wa SBL,
Simu: +255 685 260901
Barua Pepe: Rispa.Hatibu@diageo.com
Email: Rispa.Hatibu@diageo.com
No comments:
Post a Comment