Mawakala wa TCB wakifuatilia kwa umakini mafunzo hayo.
Tanzania Commercial Bank imetoa semina kwa mawakala wake zaidi ya 1,300 wanaotoa huduma za kifedha maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam, lengo likiwa ni kuboresha huduma na ufanisi kwa wateja wa TCB wanaojipatia huduma za kibenki kwa mawakala hao.
Akizungumza katika semina hiyo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania Commercial Bank, Bw. Jema Msuya alisema semina hizo ni mwendelezo wa mafunzo kwa mawakala waTCB nchi nzima ili kuboresha huduma, kukuza biashara zao na kuleta ufanisi kuboresha katika kumuhudumia mteja.
Alisema TCB hadi sasa tumekuwa na mawakala zaidi ya 5,600 ambao hutoa huduma nchi nzima huku ikiwa na matawi 82 na mashine za ATM zaidi ya 400 lengo likiwa kusogeza huduma kwa wateja wake.
Jema alisema huduma ya TCB Wakala iliyoanzishwa ili kusaidia na kuondoa kero mbalimbali kwa wateja wa TCB ikiwemo foleni katika matawi mbalimbali ya benki hiyo huku ikitoa ajira kwa mawakala zaidi ya elfu 5,600 ambao nao wameajiri vijana mbalimbali ambao wanajipatia kipato.
Mafunzo haya yanaenda sambamba na kuwapongeza mawakala waliofanya vizuri kwa mwaka huu katika kazi zao, ili kuleta chachu kwa wengine kufanya vizuri zaidi.
Kwa upande wake, mmoja ya mawakala Raqeeb Hamidu ameishukuru TCB kwa kuandaa semina hizi mara kwa mara kwa sababu wanazidi kunufaika na kuongeza uwezo wa kuwahudumia wateja kwa uadilifu mkubwa na wepesi.
Tanzania Commercial Bank imekuwa Benki ya kwanza kwa kutujali sisi mawakala na wateja wake maana hizi semina zinakwenda kumsaidia wakala wa zamani lakini pia wakala wapya.
No comments:
Post a Comment