Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation imetangaza ushirikiano na waendesha baiskeli mashuhuri wa TwendeButiama kama mdhamini mkuu wa tukio lao la kila mwaka la ziara ya Baiskeli inayoanzia jijini Dar es Salaam mpaka Butiama mkoani Mara. Tukio hili la uendeshaji wa baiskeli litakalodumu kwa siku 14, linatarajiwa kufanyika kuanzia tarehe mosi mpaka 14 Oktoba mwaka huu, likitumika kama heshima ya maisha na kumbukumbu ya kumuenzi Hayati Baba wa Taifa, Mwl Julius Kambarage Nyerere, mtu muhimu katika historia ya Watanzania.
Mbali na kuchangia garama zote za uendeshaji kwa ajili ya msafara huu kuelekea Butiama, Vodacom Tanzania Foundation imejipanga kushiriki kwenye shughuli tofauti zinazoendana na mkakati wao wa kuleta mabadiliko kwa kuboresha huduma za afya, upatikanaji wa elimu bora na uwezeshaji wa kiuchumi kwa garama ya zaidi ya millioni 200.
“Tutaungana na waendesha baiskeli wa TwendeButiama kuchangia madawati katika shule 5 na kupanda miche ya miti zaidi ya 4,000 katika mikoa tofauti ambayo waendesha baiskeli watapita. Shughuli hii inaendana na mkakati wetu wa kupanda miti milioni 2 nchini kote ifikapo mwaka 2030. Kwa kuongezea, tunashirikiana na ‘Afya Checkers’ ambao ni wataalamu wa huduma ya afya kuandaa kambi maalum zitakazotoa huduma ya upimaji, matibabu ya bure na pia kuwapa rufaa wagonjwa katika maeneo ya Mwanza, Bunda, na Butiama ikiwa ni juhudi zetu za kupambana na magonjwa ya kuambukiza nchini, vilevile tutachangia vifaa tiba katika Hospitali ya Wilaya ya Butiama,” alisema Bi. Farah.
Kwa upande wake Dr. Romana Malikusema akizungumza kwa niaba ya wataalamu wa afya ambao watakuwa sehemu ya ufanikishaji wa Kambi ya Matibabu ya bure ameishukuru Vodacom Tanzania Foundation kwa kuwaunga mkono kuhakikisha zoezi la kambi hizo linafanikiwa kwa wakazi wa Mwanza, Bunda na Butiama.
“Tunayofuraha kuwa sehemu ya ziara ya Baiskeli ya TwendeButiama kuenzi kumbukumbu ya Mwalimu kupitia uwezeshaji wa kambi ya matibabu ya bure. Mwalimu Nyerere alijitolea kupambana na magonjwa nchini Tanzania na tunatarajia kusaidia na kuwahudumia watu wengi kadri tuwezavyo. Tutakuwa wataalamu wa afya kama manesi, madaktari na wataalam wa lishe watakaowahudumia na kuwashauri watu ambao watahudhuria. Ningependa kutoa wito kwa washirika wengi Zaidi kujitokeza ili kuunga mkono jitihada hizi za kipekee zinazolenga kugusa Maisha ya watu wengi Zaidi,” aliongeza Dkt Malikusema.
Kwa taarifa zaidi kuhusu ziara hii, tafadhali tembelea (http://www.twendebutiama.com).
Kuhusu Vodacom Tanzania Foundation:
Vodacom Tanzania Foundation ni sehemu ya Vodacom Tanzania PLC iliyojikita katika miradi ya kusaidia jamii kwa kutimiza wajibu wake wa kuunufaisha umma hususani makubdi yasiyojiweza hususani wanawake na vijana. Taasisi inajumuisha misaada ya kijamii kwa kutumia teknolojia ya mawasiliano ya simu za mkononi kutoa ufumbuzi kwa changamoto mbalimbali za kijamii.
Kwa kufanya kazi na taasisi za ndani zisizo za kiserikali na washirika, mpaka sasa taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation imeunga mkono zaidi ya miradi 120 kwa kuwekeza zaidi ya TZS 15 bilioni kuboresha Maisha ya Watanzania.
Kwa taarifa zaidi, tafadhali tembelea:
https://vodacom.co.tz/en/vodacom_foundation_aboutus/?SID=1u5nsmti8ahqks35k9tds71652
No comments:
Post a Comment